Mkurugenzi wa Chuo cha Uhazili cha Splendid cha Ilala akivishwa skafu na skauti Ramadhani Juma akimkaribisha shule ya Sekondari Abuu Jumaa ya Kivule Kitunda Dar es Salaam ambako alikuwa mgeni rasmo katika mahafali ya kumaliza kidato cha Nne mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari ya Abuu Jumaa Kitunda Kivule akimkabidhi cheti mewanafunzi hadija Hamisi katika sherehe iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
WANAFUNZI Kumi yatima wanaomaliza kidato cha Nne Shule ya Sekondari ya Abuu Jumaa YA Kivule,Ilala Dar es Salaam wamepatiwa nafasi ya kusoma bure mafunzo ya Komputa katika Chuo cha Slendid Cha Ilala Bungoini.
Mkurugenzi wa Chuo cha Uhazili cha Splendid Bw Cassim Taalib ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafani ya nne ya shule hiyo alisema jana Dar es Salaam jana kuwa wanafunzi hao wamepewa nafasi hiyo ikiwa na mchango wa mkurugenzi huyo kusaidia wanafunzi wenye shida.
Bw.Taalib aliwataka wanafunzi wanaoanza mitihani yao Novemba 4,mwaka huu wajitahidi kujibu maswali kama wanavyoulizwa na wasikate tamaa kwani elimu haina mwisho wasikate tamaa bali wajiendeleze kusoma na kuahidi kutoza nusu ada kwa wanafunzi wanaotaka kusomea komputa kwenye chuo chake.
Aliwataka wazazi kuchangia elimu ya watoto kwani changamoto nyingi zinazowakwaza watoto washindwe kuendelea na masomo kunatokana na wazazi kutochangia michango ya watoto wao na kushindwa kujua maendeleo ya watoto wao.
"Nninawaambieni Kama mzazi, mtoto asiposoma anaharibika,kati ya 300 walioanza kusoma wanafunzi wanaomaliza masomo ninaowakabidhi vyeti ni 187, waliobaki wengine wamehama na wengine kuacha shule lakini mkianza safari ya wote ni vizuri mmalize wote"alisema Bw. Taalib.
Katika risala ya shule ya Sekondari Abuu Jumaa, walisema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwepo kutokuwa na umeme ambao unawanyima fursa ya kujifunza komputa na kutokuwa na maji katika shule hiyo licha ya wahisani kuwachimbia kisima cha maji kinachohitaji pampu ya umeme kutoa maji.
Pia walisema shule hiyo inakabiliwa na utoro wa wanafunzi kutokana na kukosa ukuta wa kuzunguka shule na kukabiliwa na uhaba wa walimu hasa wa masomo ya sayansi na hawana vyumba vya maabara kwa ajili ya masomo ya baiolojia na sayansi.
Makamu Mwenyekiti wa shule hiyo, Bw. John Roko alisema jitahada zinafanyika kushirikiana na walimu wa shule hiyo kuhakikisha kuwa changamoto zinazowakabili kunatafutiwa ufumbuzi.
Alisema bado kunachangamoto ya wazazi kusuasua kutoa michango ya shule kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kunakochangia shule kushindwa kujiendesha na kukamilisha mipango waliojiandalia kuboresha huduma katika shule hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...