WAZIRI
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amewataka
Watanzania kujenga utamaduni wa kupima afya zao kabla ya kuugua pamoja
na kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili wanufaike na
huduma zake.
Rai
hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) ambao uliendesha zoezi la upimaji wa afya za wananchi
bure katika maonesho ya Tanzania Homes Expo.
“Ni
vyema kwa kila mtanzania anapopata fursa kama hii akaitumia ili kujua
afya yake hususan nyie wanahabari ambao ndio mmekuwa mstari wa mbele
kuzifahamu hizi fursa, mtu ukijua afya yako ni rahisi kujikinga na
magonjwa mengine hasa yasiyoambukizwa” alisema Prof. Mbarawa.
Waziri
huyo ambaye naye alitumia fursa hiyo kupima afya yake na kupata ushauri
wa kiafya kwa watalaam, aliupongeza Mfuko wa juhudi mbalimbali ambazo
umekuwa ukifanya katika kutoa na kuboresha huduma za afya kwa
Watanzania.
Katika
maonesho hayo ya siku mbili wananchi wengi wamepata huduma ya kupima
afya zao na kupata ushauri ambao unalenga kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza.
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa ukiendesha upimaji wa afya katika
maeneo mbalimbali unaoambatana na utoaji elimu ya kujiunga na Mfuko huo
pamoja na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mifuko ambayo inapunguza mzigo
mkubwa wa kugharamia matibabu kwa wananchi ambao wamejiunga nao.
Akizungumza
katika maonesho hayo, Meneja Masoko wa Mfuko huo, Angela Mziray
aliwataka watanzania kujiunga na NHIF ili wanufaike na mafao yake
likiwemo fao la wastaafu ambao wanatibiwa bure kwa maisha yao yote.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akipima
urefu katika banda la NHIF katika maonesho ya Tanzania Homes Expo
yanayofanyika Mlimani City Dar es Salaam.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akisaini
kitabu cha wageni katika banda hilo baada ya kupima afya yake.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda hilo kwa lengo la kupima na kupata elimu ya Mfuko huo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...