
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo katikati akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia kwake, Mbunge wa Nkasi Kusini Ally Kessy kushoto kwake na wazee wawili kulia na kushoto wakiwawakilisha wananchi wa Namanyere (Wilaya ya Nkasi) katika uzinduzi rami wa mradi wa umeme kutoka Sumbawanga hadi Namanyere Wilayani Nkasi tarehe 28, Oktoba 2013. Mradi huo uliogharamiwa na Serikali ya Tanzania na kukamilika hivi karibuni una gharama ya Tsh. Bilioni 4.3 na umepitia jumla ya vijiji kumi na mbili vya njiani kabla ya kutua katika Mji huo wa Namanyere uliopo Wialayani Nkasi Mkoani Rukwa. Tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na tangu kuundwa kwa Mkoa wa Rukwa mwaka 1974 Wilaya hiyo haikuwa na umeme jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe na wananchi wa Wilaya hiyo.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na washirika wake katika uzinduzi huo wakibofya kitufe maalum kama ishara ya kuwasha umeme katika Mji wa Namanyere tarehe 28, Oktoba 2013 baada ya Wilaya hiyo kukosa huduma hiyo katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Katika uzinduzi huo Prof. Muhongo amesema Mkoa wa Rukwa umetengewa zaidi ya Tsh. bilioni 30 kwa ajili ya umeme vijijini kupitia REA, Wakala wa Umeme Vijijini ambapo jumla ya vijiji 66 katika kipindi cha miezi 20 ijayo kuanzia Novemba mwaka huu 2013 vitanufaika na mradi huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Hongera Bongo
ReplyDeleteThis is what I call progress
Sumbawanga kulikuwa hakuna umeme, hata huko hospitali ya mkoa operesheni zote zilikuwa ni lazima zifanywe mchana, na kwenye emergency usiku, the theatre lamp had alligator clips to connect it to the battery of a Land Rover parked outside.