Ubalozi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata
fursa kuja kuzungumza na Waziri wa Sheria na Katiba, Mheshimiwa Mathias Chikawe na Wawakilishi kutoka
Wizara
ya Sheria na Katiba - Tanzania, hapa Ubalozini siku ya Ijumaa (tarehe 01
Novemba 2013) kuanzia saa Tisa alasiri (15:00).
Mheshimiwa Waziri anatarajiwa
kuzungumzia masuala mbalimbali ya Sheria na mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya
Tanzania unaondelea hivi sasa.
Mhe. Waziri Chikawe anatarajiwa
kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi watakaohudhuria mkutano huo.
IMETOLEWA
NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA
MIMI NAKWENDA KUPIGA MABOX LONDON UNDERGROUND NIKIMALIZA MAPEMA NITAKIJA.MDAU LUTON.
ReplyDelete