Wilfred Moshi na Mlima Everest, inazungumzia safari ya kusisimua na kutisha ya kijana shujaa wa Kitanzania anayefanya kazi ya upagazi kuhudumia watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro. 
 Wilfred aliyaweka maisha yake rehani ili kuweka rekodi mpya kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest ambao ni mrefu kuliko yote duniani na kuiletea Tanzania sifa kubwa kimataifa. Urban Pulse Creative Media, Freddy Macha wakishirikiana na Ubalozi wetu Uingereza wanakuletea habari hii ya kusisimua kwa majuma matano mfufulizo ili tuone na kujifunza kutokana safari yake ya hatari. Asanteni, 
 Urban Pulse Creative, Freddy Macha 
na Ubalozi wa Tanzania, Uingereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera sana. I hope he makes it to the very top. Very few have made it and would certainly be the first TZ person to succeed. But if up to base camp, then he will be second Tz person. Just to add that it is not easy to get to base camp. Quite dangerous actually. So i am praying that this chap concurs it. All the very best. Keep us updated with progress.

    ReplyDelete
  2. Hongera Sana Wilfred Moshi Ur The HERO bRO

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwako, familia na nchi ya Tz kwa ujumla kwani umeipeperusha bendera ya Tz. Mungu akuzidishie pale ulipopunguza kwa kujitolea, hakika wewe ni shujaa wa kuwekwa kwenye kumbukumbu nzuri za historia ya Tanzania kwa vizazi vijavyo. Vitabu vitakuandika mana umeweka historia. Mdau hapo juu msikilize na sio kukisia kama ameishia base camp yeye ni wa pili, si usikilize mpaka mwisho! amefika kileleni mpe hongera anastahili huyo kaka, inapobidi kusifia tusifie jamani. Ila watanzania wengi wana mawivu yasiyo na maana. Hongera sana sana Mushi.

    ReplyDelete
  4. Amefika au vipi? Tunaomba update.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...