Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto) akimpongeza mchezaji wa riadha wa Mambo ya Ndani Sports Klabu baada ya kumvisha medali mchezaji huyo katika hafla ya kufunga Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi kikombe cha ushindi Kapteni wa timu ya Kuvuta Kamba Wanaume ya Mambo ya Ndani Sports Klabu baada ya timu hiyo kuibuka mshindi wa pili katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Mambo ya Ndani Sports Klabu wakipita kwa maandamano mbele ya Jukwaa Kuu la Mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kulia)akisalimiana na wachezaji wa timu ya mchezo wa Kuvuta Kamba ya Mambo ya Ndani Sports Klabu, alipokuwa akikagua timu za michezo zilizoshiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Mambo ya Ndani Sports Klabu baada ya kutwaa vikombe vitatu na medali 3, mbili zikiwa za dhahabu na moja ya fedha katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Nigel Msangi. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...