Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto) akikagua ujenzi wa maabara ya kisasa ya Sekondari ya
Mdandamo iliyopo katika Kata ya Mletele, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa
ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo
iliyopo jimboni mwake.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (watatu kushoto) akiwa na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa
ya Songea, Madiwani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilayani humo wakati
walipokuwa wanakagua ujenzi wa maabara, mabweni pamoja na nyumba za walimu wa
Shule ya Sekondari ya Mdandamo iliyopo katika Kata ya Mletele, Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano
akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni
mwake.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (aliyevaa mawani) akiwa na Watendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Songea, Madiwani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani
humo wakilikagua daraja lililopo katika Kata ya Mletele ambalo lipo hatua ya
mwisho kukamilika. Hata hivyo, Dk Nchimbi alichangia Shilingi milioni moja kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja hilo. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa
ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo
iliyopo jimboni mwake.
Msanii
maarufu wa kuigiza sauti mbalimbali za Viongozi wa Serikali, wanasisa,
watangazaji wa habari za kwenye Luninga na redio, pamoja na wasanii mbalimbali
nchini, Adamu kwa jina maarufu ‘Mlugaluga’ akitoa burudani kwa wananchi wa Mtaa
wa Liwumbu, Kata ya Mletele, Manispaa ya Songea kabla ya Mbunge wa Jimbo la
Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi (kulia) kuzungumza na wananchi hao kuhusiana na masuala mbalimbali ya
maendeleo ya kata hiyo. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano
akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Matarawe, Mjini
Songea kuhusiana na masuala mbalimbali ya maendeleo ya kata hiyo, hata hivyo Dk
Nchimbi aliwahakikishia wananchi wake kuwa, kwa kushirikiana na Watendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Songea watalitengeza Daraja la Matarawe ambalo mara
kwa mara linasababisha ajali mbalimbali zikiwemo za bodaboda. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku
tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni
mwake. Picha zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...