Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.

Katika mazungumzo, Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho kukamilisha majadiliano ya mikataba ya Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja ikiwa ni masuala ya Kilimo, Maendeleo na Uwezeshaji Biashara.

Aidha, Mkurungenzi Mkuu alielezea mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu, na kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu.

Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyo nayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali Indonesia kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo matatu yaliyotajwa hapa juu.
Balozi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo.
Balozi Mero na Bw. Azevedo katika mazungumzo.
Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hizi ni zama za BRICS.

    Kwa waliofuatilia Siasa za Biashara za Kimataifa mwaka huu 2013 mwezi wa June hivi palifanyika Uchaguzi Mkuu ktk Shirikisho la Kimataifa la Biashara WTO ktk Makao Makuu yake huko Geneva-Uswisi.

    Miaka nenda miaka rudi Shirikisho limekuwa chini ya Wakurugenzi Wakuu kutokea nchi za Magharibi Ulaya na Marekani ya Kaskazini.

    Kama ilivyo kuwa Hulka za Kisiasa popote pana Kautamaduni kwa kujipendelea Kimaslahi, na ndivyo ilivyokuwa ktk Shirikisho la WTO kitu ambacho kilikuwa kinafanywa na Wakuu wengi waliotokea nchi hizo za Magharibi, kwa kutoa Vipaumbele vya Biashara kwa upendeleo wa nchi na maeneo yao.

    Lakini safari hii mambo yamebadilika na Uchaguzi huu WTO imeangukia mikononi mwa Mkuu kutoka Kundi la nchi za BRICS nchi za Brazil,Russia,India,China and South Africa.

    Kama zilivyo dhalimu nyingi hazikosi Vibaraka, ktk hilo Uganda wamekuwa ni Mawakala kwa kuwa na Mfumo wa Biashara wa MULTI LATERAL TRADING SYSTEM ndio maana Mgombea wa Kundi la WEST Dr.Herminio Blanco wa Mexico laifika Kampala waklati wa Mchakao wa Kampeni za Uchaguzi huo na huku aliyekuwa Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu alitokea nchi jirani yetu Rwanda Bi. Valentine Rugwabiza ambaye kwa sasa baada ya kung'oka huko WTO amerudi Kigali anaongoza RDB-Rwanda Development Board.

    Hivyo ktk Afrika ya Mashariki Uganda na Rwanda wangenufaika na West kulingana na Mfumo wao wa Biashara huku Tanzania, Kenya na Burundi zikinufaika na BRICS kutokana na mfumo wao wa biashara.

    Na ndio sasa tunashuhudia huyu Roberto Azevedo kutoka Brazil (Brics) akiwa ndio Mkurugenzi Mkuu mpya!

    ReplyDelete
  2. Commentator na 1 kachanganyikiwa!!! Kila kitu kina mahala pake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...