Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika mnamo tarehe 24/12/2013 mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.
Picha zaidi za Mwanamuziki mkali Afrika akisaini mkataba baina yake na viongozi waandaaji wa Show hiyo. Makubaliano haya ya kuweka mkataba yamefanyika jumatatu ya wiki hii tarehe 25/11/2013 jijini Kampalanchini Uganda.
Mwanamuziki Dr. Jose Chameleone (katikati) akiwa na Mapromota wa show itakayofanyika jijini Mwanza Dennis Mshema (Kushoto) na Mr. Ben Mwangi (kulia) mara baada ya utiaji wa saini wa kupiga show moja kali tena takatifu itakayofanyika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas katika uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
 Kwa mujibu wa moja wa Mapromota hao Mr. Ben amesema kuwa ile kiu ya mashabiki wa muziki wa ukweli toka kwa Mwanamuziki Jose Chameleone sasa inakwenda kupata dawa yake, kwani maandalizi mazuri yameanza kufanyika kuhakikisha kila kilichobora kina tukia kwenye jukwaa la burudani siku hiyo ya mkesha wa Christmas.

"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Alisema Ben.

 Ameongeza kuwa bado milango iko wazi kwa makampuni mbalimbali na sekta binafsi kushiriki katika suala zima la udhamini. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0752813212.

Mbali na kuwa na masongi makali kama Bei kali, Kamila na kadhalika ambayo hadi sasa utamu wake uko pale pale Jose Chameleone kwa sasa anatikisa ulimwengu wa burudani ya muziki na ngoma zake kali kama Badilisha, Sumula, Valu valu, Tubonge na nyingine kibao... 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Go North, go west make your Ugandan Government take isolation of the 'Coalition of the willing' whatever the case POLITICALLY ECONOMICALLY, SOCIALLY TANZANIA REMAIN THE EAC's CENTRE OF GRAVITY !

    Mtatutenga mtafanya mengi dhidi ya Tanzania lakini itabaki Tanzania kuwa Mhimili wa Africa ya Mashariki!

    Chameleone Karibu sana Tanzania, NTUMBANI NDANI YA AFRIKA YA MASHARIKI yetu utumbuize na kutuliwaza kwa X-Mass !!!

    ReplyDelete
  2. Hahahaha Mdau wa kwanza hilo 'Dubwana' la CoW limesha fariki dunia wenyewe wanakanyagana sana na wanajipanga jinsi ya kujieleza ktk Mkutano kesho Jijini Kampala Uganda!

    Ni jambo lilikuwa la ajabu sana hadi Wadau wengi wa Afrika ya Mashariki Wakenya, Waganda,Warundi na Warwanda wengi waliopo nje waishangaa sana EAC bila Tanzania ingekuwa ni kituko!

    ReplyDelete
  3. Kikwete Dakitari Bingwa Afrika ya Mashariki!

    Tushukuru sana ya kuwa Afrika ya Mashariki ina Dakitari wake Bingwa sio mwingine bali ni Mhe. Raisi Jakaya Kikwete !

    Mgonjwa alipatwa na Kirusi cha Utengano wa CoW lakini Dakitari alimpima Mgonjwa Kitaalamu akagundua anasumbuliwa na Ugonjwa huo na ile tarehe 7 Novemba 2013 akiwa Dodoma Dakitari alimzamisha Mgonjwa (Afrika ya Mashariki-CoW) SINDANO YA TIBA kwa njia ya Hotuba na sasa tunashukuru Mgonjwa amekaribia kabisa kupona!!!.

    Na kesho tunatarajia huko Kampala Uganda Dakitari atazamisha Sindano ya mwisho kwa Mgonjwa (EAC-CoW) na tunatarajia amatakuwa ameruhusiwa kutoka Hospitalini atapitia Rwanda kusalimia akiwa amepona na afya yake njema!!!

    ReplyDelete
  4. Anatingisha ndani ya mwanza tu,huku kwetu morogoro wala hatii mguu coz vipaji vya kutisha na wala hatubabaikii mtu au watu wa kutoka taifa lingine huku sisi na Afande sele tu na wadogo zake kama vile Stamina,Bele 9,na wengine wakumwaga,,Afande Sele 10-huyo mapepe wenu 0,,,Mwanza punguzeni ushamba muwe mnamkumbuka mtu wenu FID Q

    ReplyDelete
  5. we chameleon usije ukakimbia na ela za watu tena, nafikiri umejifunza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...