
Viongozi wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi wakionyesha hundi yenye thamani ya shilingi milioni nane waliyopewa na COSTECH kama "Seed Fund" kwa ajili kuendeleza kongano la wafugaji Wilayani humo. Kulia wanaoshuhudia ni Ndugu Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa COSTECH na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi (hawako pichani) katika Mkutano uliofanyika Kalambo Ranch Wilayani humo tarehe 14 Novemba 2013. Mkuu huyo Mkoa aliwataka wafugaji kufuga kisasa bila kuathiri mazingira kwa kufuga mifugo michache inayoendana na maeneo husika, aliwataka pia wafugaji kuwaendeleza watoto wao kielimu tofauti na ilivyo hivi sasa amabao wengi wao hufanyishwa kazi za uchungaji wa mifugo. Katika hotuba yake fupi alitoa agizo kwa halmashauri zote Mkoani Rukwa kuweka kipaombele katika kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima katika kila kijiji na kujiwekea mkakati wa idadi ya mifugo itakayofugwa kulingana na ukubwa wa eneo la malisho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi Ndugu Pancras Maliyatabu Cheti rasmi cha usajili wa umoja huo uliosajiliwa rasmi tarehe 30 Agosti 2013. Katikati anaeshuhudia ni Katibu wa umoja huo ndugu Jisena Biliya.
Picha ya pamoja.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...