Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Viongozi mbali mbali, wakipata maelezo ya ujenzi wa Barabara za Wilaya ya Wete,zikiwemo Kipangani-Kangani,Chwale- Likoni,na nyengine zinazojengwa kwa ufadhili wa Shirika la MCC la Marekani,kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu,Injinia R.D.Sharma,wa kampuni ya Lea Associates south Asia PVT,wakati wa ziara ya Wilaya ya Wete Pemba.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza pamoja na wananchi wa Mzambarau Takao,baada ya kupata taarifa za Ujenzi wa Barabara za Wilaya ya Wete zinazojengwa na mfuko huo jana akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mzambarau Takao,alipokuwa katika ziara ya kuzitembelea Barabara zilizojengwa na Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC katika Wilaya ya Wete , Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,(kulia ya Rais ) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ,Haji Omar Kheir.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...