Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...