Kwanza kabisa naomba nisieleweke vibaya kwa kuwa ninaamini kwamba Kila tendo ambalo linaenda kinyume na sheria katika jamii ni lazima sheria ichukue mkondo wake, na kwa kuwa mahakama iliamua beyond resonnable doubt kwamba hawa jamaa walithibitika kutenda makosa hayo na walistahili adhabu ambayo wanatumikia. Kwa hili ninaiheshimu mahakama na maamuzi yake.
Ila kikubwa ambacho nataka kukiongelelea hapa ni kuhusu wasanii na watu mbalimbali ambao kichinichini wamekuwa wakijifanya kuwaonea huruma na kufikiri kwamba hawakutenda bila kuchukua hatua zozote za kimsingi za kuwasaidia hawa jamaa zaidi ya kupiga kelele za chini ya uvungi zisizosaidia.
Kimuziki mimi binafsi nilikuwa na bado ni mshabiki mkubwa sana wa PAPII KOCHA na baba yake, sifurahii kama ni kweli walitenda makosa hayo katika maisha yao binafsi. Lakini hii haijalishi mapenzi yako kwa vipaji vyao.
Sasa nakuja kwa Hawa wasanii na watu wengine wenye mapenzi na hawa watu na Hasa wale wanaoamini kwamba jamaa walionewa katika hili huko nyumbani Tanzania.
Hivi kweli wameshindwa kuunda umoja wenye sauti na kuandika barua yenye nguvu kwa Rais ya kuwaombea msamaha hawa jamaa? Hivi kweli wasanii wote wa Tanzania wakiungana na kutia sahihi katika barua (Petition) ya kuwaombea msamaha wa Raisi hawa jamaa wether walitenda au hawakutenda kosa.
Hivi mnafikiri kweli Raisi wetu hatalifikiria hili? kwa mawazo yangu mimi nahisi there is 75% chance ya Rais kufanya kitu kama akiombwa na sauti ya wengi hasa wasanii ambao CCM Inawategemea sana hasa katika nyakati hizi za kuelekea kwenye uchaguzi.
Sisemi kwamba watu hawajafanya kitu kuwasaidia hawa jamaa, naamini kuna watu wamekuwa hawalali kuwahangaikia hawa jamaa lakini nguvu yao haijatosha na sauti yao haijasikika.
Ila naamini fika kama Wasanii wote wenye mapenzi mema ya vipaji na moyo wa kusaidia na kusamehe wakiungana na kupeleka tamko rasmi la maombi ya kimaandishi yenye sahihi za wote ya kuwaombea msamaha hawa jamaa kwa
Muheshimiwa Raisi wetu kipenzi Jakaya Mirisho Kikwete atawafikiria na kidogo au kikubwa kitafanyika.
NAOMBA KAMA UMEUPENDA WARAKA HUU U-REPOST, SHARE NA USAMBAZE KWA WAHUSIKA HASA WASANII NA VIONGOZI WA WASANII HUKO NYUMBANI TANZANIA.
<<FROM DJ KAYCEE, HOUSTON TEXAS, USA.>>
Hakuna msamaha kwa wabakaji
ReplyDeletekwanini usianze wewe kuja Bongo kuwaombea msamaha.Hivi unajua polisi wa Bongo??
ReplyDeleteWe mdau! acha sheria ichukue mkondo wake! Najua ndugu na marafiki wanasikitika kwamba wako mbaroni hawa jamaa lakini kuna wale waliofanyiwa unyama ambao hawatakaa wasahau. Nafikir kifungo hiki kitakomesha mapepo mengine kama haya. Hivi angekuwa mtoto wako amelawitiwa ungependekeza wapewe msamaha!
ReplyDeleteNyie ndio mnadhalilisha sheria za nchi.
They were both convicted by the court and what you are propagating on this blog is wrong. Celebrities or politicians should not be excluded from the law of the land. I am saddened by the fact that this article was written by someone that lives in America with a doctorate degree. SMH!
ReplyDeleteDo you think about the children that were molested? Do you still have same African mentality in the states that with social status one can get away with things? It was only last week that a Tanzania cabinet minister was accused of raping and giving a student HIV without any consequences. The Oyster Bay Police made an arrangement for him to pay living expenses without prosecuting him. Tanzania needs more children and women activists as educated people like you are not helping the situation.
Hivi angebakwa mtoto wako wa miaka saba je ungewaombea msamaha? Walirudia vitendo vyao vya kinyama si mara moja wala mbili. Hakuna msamaha
ReplyDeleteWaasi wa Congo wanatumia sana "Ulawiti" kama silaha.
ReplyDeleteNakumbuka niliwahi kuongea na askari mmoja aliyehusika katika upelelezi wa kesi hii, akaniambia kuwa mmoja wa wazazi wa watoto waliofanyiwa unyama huu alizimia wakati mwanae akieleza yale aliyofanyiwa na hawa watu. Kwa sababu za kimaadili nisingependa kuandika hayo hapa.
ReplyDeleteKwanza nadhani ni dhana potofu kuendelea kuamini kuwa hawa watu walionewa/wanaonewa. Binafsi siamini kama kweli Mahakama ya Hakimu Mkazi mpaka Mahakama ya Rufaa wawe tu wanawakandamiza hawa watu. Kwa kuwa walipatikana na hatia na mahakama zote zimekubaliana hivyo, huo ndiyo ukweli wa suala hili. Kwa kuwa tukio hilo lilitokea Sinza, sioni kwa nini mtu usifanye utafiti kwa kufika huko kupata ukweli wa tukio hilo?
Mimi nimeshangazwa sana na hoja iliyotolewa, eti kwa sababu watu hao wanapendwa na watanzania wengi basi waombewe msamaha, vipi wale ndugu zetu ambao hawafahamiki kwa watanzania, wao wasiombewe msahmaha? Kwa maoni yangu, kwa kuwa watu hawa walipaswa kuwa mfano kwa jamii yetu, hawasitahili kupewa msahama ili sisi tuliopata nafasi ya kuheshimika kijamii tujifunze ili tusiige mfano wao. Haki inapaswa kuonekana inatendeka kwa wote bila kujali nafasi zao katika jamii, lakini wale wenye nafasi wanao wajibu wa kuwa mfano kwa wengine.
Kama wewe ni mzazi na mwanao hajawahi kufanyiwa unyama huo, mshukuru Mungu na kuendelea kumuomba Mungu awalinde wanao wasije wakapatwa na jambo hilo. Lakini kwa wale waliowahi ama kufanyiwa unyama kama huu au ndugu zao/watoto wao walifanyiwa unyama wa aina hii watahuzunika na kuumia sana siku wakisikia kuwa Rais wetu mpendwa amewasamehe watu hawa, ingawa nadhani sheria haimruhusu Rais kutoa msamaha kwa wabakaji.
Nakumbuka niliwahi kuongea na askari mmoja aliyehusika katika upelelezi wa kesi hii, akaniambia kuwa mmoja wa wazazi wa watoto waliofanyiwa unyama huu alizimia wakati mwanae akieleza yale aliyofanyiwa na hawa watu. Kwa sababu za kimaadili nisingependa kuandika hayo hapa.
ReplyDeleteKwanza nadhani ni dhana potofu kuendelea kuamini kuwa hawa watu walionewa/wanaonewa. Binafsi siamini kama kweli Mahakama ya Hakimu Mkazi mpaka Mahakama ya Rufaa wawe tu wanawakandamiza hawa watu. Kwa kuwa walipatikana na hatia na mahakama zote zimekubaliana hivyo, huo ndiyo ukweli wa suala hili. Kwa kuwa tukio hilo lilitokea Sinza, sioni kwa nini mtu usifanye utafiti kwa kufika huko kupata ukweli wa tukio hilo?
Mimi nimeshangazwa sana na hoja iliyotolewa, eti kwa sababu watu hao wanapendwa na watanzania wengi basi waombewe msamaha, vipi wale ndugu zetu ambao hawafahamiki kwa watanzania, wao wasiombewe msahmaha? Kwa maoni yangu, kwa kuwa watu hawa walipaswa kuwa mfano kwa jamii yetu, hawasitahili kupewa msahama ili sisi tuliopata nafasi ya kuheshimika kijamii tujifunze ili tusiige mfano wao. Haki inapaswa kuonekana inatendeka kwa wote bila kujali nafasi zao katika jamii, lakini wale wenye nafasi wanao wajibu wa kuwa mfano kwa wengine.
Kama wewe ni mzazi na mwanao hajawahi kufanyiwa unyama huo, mshukuru Mungu na kuendelea kumuomba Mungu awalinde wanao wasije wakapatwa na jambo hilo. Lakini kwa wale waliowahi ama kufanyiwa unyama kama huu au ndugu zao/watoto wao walifanyiwa unyama wa aina hii watahuzunika na kuumia sana siku wakisikia kuwa Rais wetu mpendwa amewasamehe watu hawa, ingawa nadhani sheria haimruhusu Rais kutoa msamaha kwa wabakaji.
Kila siku watu wanabakwa, hata huko Marekani alipo mtoa hoja kuwa ubakaji. Kila siku tunavilaumu vyombo vya sheria vinakaa kimya, sasa watu wametiwa hatiani, tunalalama! Hivi tutapunguzaje ukabaji unaoendelea kila siku?
mimi naomba na wabakaji na walawiti wengine kesi zao ziende speed wafungwe, huko ndio kunakowafaa ili wabadilike baada ya kuonja kifungo. nje watatenda makosa hayo hayo. bora hata kungekuwa na adhabu kali zaidi kama za kule nchi nyingine ambapo hata wauza unga huwa wananyongwa. watoto hawana mahali salama, shule shida, njiani shida na hata majumbani shida. funga wote tu. hakuna cha kuombewa msamaha wala nini, tena mimi ntaomba petition ipite kuwa wasanii wanaomba kesi za namna hiyo ziamuliwe haraka. chezea mkono wa sharia wewe! kuna nchi mpaka ubake zaidi ya mara moja ndio unafungwa; ni kama wanachochea kila mtu abake mara moja tu! wewe unaeleta hoja bakwa wewe tuone kama hutapiga kelele
ReplyDeleteNachukizwa sana na maoni ya baadhi ya watu kwamba jamaa hawa waonewe huruma, waombewe msamaha n.k. Hivi kama mtoto wako ndiye ameharibiwa ungethubutu kuwaonea huruma watu hawa? Mahakama imeshathibitisha, tena mara kadhaa, kwamba jamaa wametenda makosa--watumikie adhabu inayowastahili--hili ni funzo zuri kwa wengine wenye tamaa chafu na mapepo mabaya!! Kigezo cha vipaji vyao hakina mashiko coz huko jela wako wengi wenye vipaji mbalimbali, je wote waachiwe kwa kigezo hicho? TUACHE SHERIA IKATE PANDE ZOTE.
ReplyDeletemna uhakika kuwa walitenda kosa hilo? mbona mwalimu aliyekuwa anawapeleka watoto wanaodaiwa kuwafanyiwa hivyo, mbona yuko huru?
ReplyDeleteWee annon unaesema eti wana uhakika...uhakika umethibitishwa na mahakama ilipotoa hio adhabu au unataka uhakika utoke wapi???hao ni wabakaji kwisha...sheria ifuate mkondo wake hakuna huruma kwa wanyama hawa maana hawa sio watu kuwafanyia vitendo hivi watoto wadogo...ni wanyama tosha.
ReplyDeleteKama kweli walibaka basi Haki imetendeka, hawatakiwi kuwepo uraiani. Wale watoto waliofanyiwa vitendo hivyo na wazazi wao watajiskiaje watu hawa wakiachiwa? Tuwasamehe Kwa mabaya waliofanya, lakini wabbaki jela maana huko ndo wanapotakiwa kuwepo ili iwe fundisho Kwao na Kwa wengine wenye tabia kama hizo.
ReplyDeleteNyie no nani wakuwajaji wao mlikuwepo wakati wa tukio au kila wasemalo wenye nguvu ni kweli alowbieni kila aliyeko jela wanamakosa tafakari Kabla hujasema wengi wao hapo mna ongea mtazani mlikuwepo au stori Zimanaijua .wanaonewa tu kwa sababu binafsi
ReplyDeleteNawashangaa watu wanaowaonea huruma hawa wabakaji. Katika jamii yetu watoto wengi wanafanyiwa vitendo hivi na mabazazi kama haya.Pia nawashangaa watu ambao bado wanashindwa kuamini kuwa hawa jamaa walifanya uchafu huu. Washtakiwa walipewa fursa ya kuleta mashahidi wao wa kuwatetea, bado mahakama zote ziliwaona wana hatia labda wawalaumu mashahidi wao walioshindwa kuwatetea na kuwaokoa katika kifungo hicho katika ngazi zote kuanzia Mahakama ya Kisutu hadi Mahakama Kuu.Watu hawaamini Mahakama!! Mmahakamani ndipo ilipo sheria kama umeonewa utatoka, kama umefanya makosa utabainika. Itakumbukwa pia mwaka 2003 mara baada ya tukio hili kutokea kule Sinza,Televisheni ya Taifa TVT wakati huo iliwaonesha watoto hao wadogo 12 wa miaka 6-10 wa kike na wa kiume kila mmoja alikuwa anaeleza jinsi alivyofanyiwa na huyo mwanamuziki na watoto wake 3, kama watu hawaamini waombe mikanda ya mahojiano na watoto hao toka TBC, kwa kweli ushahidi wa watoto ulikuwa halisia, haukuwa na shaka wala hawakufundishwa. Kwa tarifa tu hawa Wacongoman kwa imani za ushirikina huwa wanatumia sana kubaka ili kujiongezea umaarufu. Kuna kesi nyingi za watu wazima kubaka watoto nchini DRC, hata askari jeshi na waasi huko Mashariki mwa Congo wanalaumiwa kwa kuwabaka wanawake na watoto kila uchao.
ReplyDeleteKesi za ubakaji, ujambazi, uhaini, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya huwa hazina msamaha wa Rais. Msiende kinyume cha katiba kwa kutaka hawa wanamuziki wasamehewe, mbona huko jela kuna wafungwa kadhaa wenye kesi za ubakaji kama hao wanamuziki, basi na wao waombewe msamaha, msamaha usiwe kwa Nguza na mtoto wake kisa ni wanamuziki. Kifungo chao kiwe ni fundisho kwa wabakaji wengine wanaotuharibia watoto wetu.
ReplyDeleteHivi kuna watu wangapi wapo ndani na tunajalidi watu wawili tu? Acheni kutumia emotions kutoa mawazo yenu. Hawa watu wamefungwa na mahakama ya sheria, wamekata rufaa wameshindwa. Sasa nini tena?? Huyu babu seya ni nani asifungwe?? Hakuna mtu aliye juu ya sheria.
ReplyDeleteNaitwa the mdudu kakakuona,,ww unaetuletea mambo ya kishetani hapa kwa Michuzi nakuombea kwa mungu ubakwe ww huko uliko ndio ujue machungu yake,,n hp ww ni mlevi wa kutupwa huko uliko na iposiku utabakwa tuu,,napia family yako ibakwe pia,,na pia nahisi ww sio mtanzania bali ni mkongo mwenzao,,ushindwe na uwe na nguvu kama PAMBA,,ila watanzania wawe na nguvu za chuma cha pua,
ReplyDeleteHuyu aliyeandika inawezakana ndio wale wale wabakaji. Hivi watoto waliobakwa umewaweka fungu gani au una kitu gani cha kuandika? Ni aibu tena hata kwa mawakili wanaowatetea. Waonewe huruma????? Tofi akwa
ReplyDelete