Mtoto wa nyoka ni nyoka. Msemo huu unaendana na juhudi za kijana Hassan, mtoto wa Marehemu TX Moshi William ambaye anaonekana kuziba pengo aliloacha baba yake ndani ya Msondo Ngoma Band ambayo kila Ijumaa jioni hufanya onesho la bure katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam chini ya udhamini wa KONYAGI.
Hii ilikuwa ni usiku wa kuamkia leo
Hii ilikuwa ni usiku wa kuamkia leo


Dogo Hassan ! kamatia hapo hapo jembe,usitoke kabisa hao ndio walezi na wazazi Baba ya Muziki, umefit sana kama kiatu na soksi
ReplyDeleteWadau
FFU
Hongera Msondo Ngoma na wadhamini KONYAGI kwa kuhakikisha muziki wa kweli yaani wa dansi unaendelea na kudumu.
ReplyDeleteMakampuni mengi yaige mfano wa KONYAGI kwa kudhamini pia bendi zingine za muziki wa ki-Tanzania wa dansi iwe bendi moja-moja au tamasha kubwa la muziki wa dansi uataoshirikisha bendi kama Msondo, Sikinde, Super-Kamanyola, FM Academia, Njenje n.k
Mdau
Muziki -wa-Dansi.
Hili wo wo wo la manjano nimelikubali, na dume wake ni mstaarabu akamwachia moshi mdogo aselebuke, na moshi mdogo big up mate, keep it up buddy. Mmenikumbusha mbali vijana Enzi zetu tukiselebuka uswahilini.
ReplyDeleteHiyo inatwa "Live Band".
ReplyDelete