Hivi ndivyo hali halisi ilivyo katika eneo la Soko Kuu la Katiakoo jijini Dar es Salaam,baada ya wafanyabiashara kugomea kutokaka biashara zao zipitie kwenye mashine za kulipia Kodi zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Wafanyabiashara hao wameamua kufunga Maduka yao na kuweka mabango kama ionekanavyo pichani hapo yakiwa na ujumbe wa kupinga matumizi ya mashine hizo.
Leo ni siku ya pili kwa wafanyabiashara hao kugoma kufanya biashara,na pia huu ni mkoa wa nne sasa baada ya Mbeya,Morogoro na Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. nafikiri wanahitaji kusikilizwa, sidhani kwamba wanagoma kulipa kodi au wanataka kukwepa kodi kwa ujumla, nadhani utaratibu wa mashine zenyewe ndio tatizo, kuna tofauti kubwa kati ya kulazimishwa kutumia hiyo machine na kulazimishwa kuinunua hiyo machine.

    ReplyDelete
  2. Haiwekeni mikoa minne yote ikawa na hoja moja, na TRA wasiwasikilize. Je, nchi zote mashine hizo hutolewa na mamlaka ya kodi? Au hii ni hapa kwetu Bongo tu. Hawajakataa kutumia mshine, bali za TRA kutokana na ughali wake. Hoja ipo hapo.

    ReplyDelete
  3. Mmezoea kukwepa kodi sasa mnaanza mgomo, kwani lazima mfanye biashara, kama hamna kwanini mng'ang'ane huko?
    Mnabahati mmezoea kudekezwa nchi hii.

    ReplyDelete
  4. Hata mimi nataka kuelewa, je ni bei ya mashine inayolalamikiwa au swala zima la kutumia mashine badala ya njia zilizokuwa zinatumika. Wanaoelewa watufahamishe shida iko wapi.

    ReplyDelete
  5. HAPA NDIO TUNAPOCHEMSHA WATANZANIA MASHINE JE TUNAJUA SERIKALI WAMEZIPATA VIPI? AU KWA GHARAMA ZIPI? MARA TUNATAKA MAENDELEO MARA TUNAYAUA WENYEWE SIO KILA KITU KULALAMIKIA SERIKALI, NI MUDA SASA WANANCHI TUBADILIKE SIE KUSEMA SERIKALI RUSHWA NA HILI TUNALO FANYA WANANCHI NI RUSHWA NDIO TUNATAKA IENDELEE. MZ.

    ReplyDelete
  6. Mlipe kodi maana TZ inabana wafanyakazi tu kuwalipisha kodi. Wafanyabiashara wanakwepa kodi. Wakati umefika kila mtu alipe kodi ili nchi ipige hatua za maendeleo.

    ReplyDelete
  7. Hata Lindi waligoma

    ReplyDelete
  8. Hawa ndio mafisadi wa nchi. Na umaskini hautaisha kwa mtaji. Wao wanataka wapate faida halafu wasilipe kodi itakuwaje.

    ReplyDelete
  9. Hawa wezi tuu serikali isilegeze kamba nchi zote zinaendelea kwa kutoa kodi na bila kutumia technologia wizi utaigubika serkali.TRA kaza buti.

    ReplyDelete
  10. Kumbe kulipa kodi halali ni kazi kweli kweli.

    Leo hii ni sisi wafanyakazii wa serikali tu ndiyo tunaofyekwa kodi bila msamaha wo wote.

    Iweje hao wafanyabiashara wakatae.

    TRA kazeni uzi tuone jee na wao wataendelea mpaka lini?

    ReplyDelete
  11. Kukataa Mashine za TRA za Kodi EFD kwa Wajanja wa Kariakoo ni dalili za kukumbuka masiah ya Ujima yaliyopita walipokuwa Kizani wakifyatua Risiti za Kuchapa Gerezani huku wakipiga Hela ndefu!

    Sasa wamebanwa wanakumbuka Ubwabwa waliokuwa ule wa mwaka 1947 !!!

    ReplyDelete
  12. Kwanini niingie gharama ya 800,000 kulipa kodi?.Kwanini hizo mashine ziharibike mara kwa mara alafu niingie gharama kuzitengeneza ili nilipe kodi?. Kwanini nilazimishwe kuikopesha serekali 800,000 ili nije kuikata serikali kwenye kodi kidogo kidogo? Kumpa mtu mkopo sini hiyari?

    Kwanini iwe ghali kulipa kodi?

    NADHANI SEREKALI ITOE MASHINE HIZO BURE

    ReplyDelete
  13. Hakuna cha bure lazima mtu agharimie hata ukipewa bure, kwani watengenezaji hawakuingia gharama? Tusipende vya bure vina gharama zake. kulipa kodi jamani ndiyo kujitegemea na kuleta maendeleo hakuna njia ya mkato.

    ReplyDelete
  14. Jamani wafanyabiashara ni wajanja sana. Wanapenda kupata faida tu bila kugharamia vitu vingine. Kama mashine wanataka kupewa bure na majengo wanayofanyia biashara wangepewa bure na sesrikali. Hii ni dalili ya kukwepa kulipa kodi na ku beep serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...