I:          UTANGULIZI 
                                   
a)          Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,
1.            Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu.  Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

Mheshimiwa Spika,
2.             Mkutano huu ulijumuisha kazi kubwa zifuatazo:

Kwanza: Kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015;

Pili: Kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2013, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments (No. 3) Bill 2013];

Tatu: Kujadili Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu wa Mwaka 2013 [The GEPF Retirement Benefit Bill, 2013]; na

Nne: Kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (The Constitutional Review Act) sura ya 83.

3.            Nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki katika Kamati ya Mipango hapa Bungeni kwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015.  Napenda kuwahakikishia kuwa, maoni na ushauri kama yalivyotolewa na Waheshimiwa Wabunge yatazingatiwa na Serikali kila moja kwa uzito wake wakati wa maandalizi ya Bajeti ya 2014/2015. Vilevile niwashukuru kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...