Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura (kulia) kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah (kushoto) ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
 Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.
  
Jamal Malinzi
Rais TFF 


Dar es Salaam 
Novemba 3, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Malinzi umeanza na VISASI na hutafika popote, soma alama za nyakati!

    ReplyDelete
  2. yap! imekua TFF ya familia, kaka, na mdogo wake mbona biashara itanoga!!

    Huyo alionesha chuki hata alipokua anakabidhiwa ofisi sura yake ilikua na hasira.

    Tusubirie matokeo yetu macho.

    ReplyDelete
  3. Malinzi soka sio ngoma kwamba utarukaruka tu, acha vinyongo, maslahi ya soka la tanzania yawe mbele, dalili za taifa kuporomoka ishaanaza kunukia, bora ukauze senene

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 4 juu huo ndio Utendaji uliotukuka kwa kuwa Malinzi hawezi kuingia Madaraka akaendelea kufuga maradhi ya Kansa yaliyokwamisha Soka la Tanzania kwa muda mrefu sana.

    Hivi Mdau umesahau hadi Raisi wetu wa nchi alishalibeba Soka kwa Udhamini na gharama kubwa sana lakini matokeo hayakuwa mazuri kutokana na Watumishi Kansa ktk Shirikisho la TFF?

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa Kwanza juu,

    Ndio ninyi mnaopewa fedha za Milangoni mkiwa Wajumbe wa TFF?

    Hawa Genge hili walikuwa na dharau sana kumbuka Kipindi kile walipokuwa wakiburuzana na Mhe. Waziri Dr.Fenella Mukangara na Naibu wake Amos Makalla, jamaa walikuwa wanajiona Wajanja sana wakisema ''Wewe Waziri usilete Sheria zako za Serikalini sisi tunajua Sheria za FIFA za Michezo ambazo haziingiliwi na Serikali''

    ReplyDelete
  6. Mara nyingi wanaoanza na visasi huwa hawafiki mbali: mfano hai ni uongozi uliochaguliwa kishikaji wa ucc udsm . Waliingia na mara moja wakaanza visasi . sasa giza nene wanatafutana hawaonani

    ReplyDelete
  7. Malinzi acha kukaribisha migogoro,usitake kurejesha enzi za FAT.Umeanza kwa pupa mno,mara utangaze msamaha,mara uwatoe wengine kwenye uongozi.Hatujui kesho utakuja na lipi.Usituchoshe,bado mapema mno

    ReplyDelete
  8. Huyu Malinzi ni bora Ndolanga au wako sawa. Sijui hata alipataje hi position kwani alitolewa kwa ku to qualify.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...