Tunaandaa vipindi vya TV na Radio vya DSE. Kwa niaba ya Soko la Hisa la DSM DSE, napenda kutoa mualiko kwa watu wachache hasa Wajasiliamali wadogo na wa kati (Small and Medium Enterprises - SME) katika mjadala wa kuhamasisha jinsi ya kupata mtaji kupitia DSE. Mjadala huu utaihusisha DSE na wataalamu wengine waliobobea katika mambo ya mitaji.
Mjadala huu utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 06-December-2013 katika Private Studio: Tancot House, 2nd Floor along Sokoine Drive just opposite Luther House or Maendeleo Bank kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.00 Mchana.
Mjadala huu ni muhimu sana na utarekodiwa na baadaye kurushwa kwenye Luninga na Radio mbalimbali.
Kama utapenda kushiriki, tafadhali sana thibitisha kwa kutuma barua pepe kwenda: mtsimbe@micronet.co.tz na pia uandike namba yako ya simu. Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...