Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Nsagali uliopo Ushirombo wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita jana.Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Masele,Wa pili kushoto ni mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bwana Emmanuel Silanga, Wanne kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mh.Profesa Kalikoyela Kahigi na kulia mwisho ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Geita Mhe. Said Magalula.
Mmoja wa Wamiliki wa Mgodi wa Ngasali Bwana Emmanuel Silanga kulia akimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete uchenjuaji wa dhahabu unaofanyika katika mgodi huo uliopo Ushirombo,Wilayani Bukombe, mkoa wa Geita. Picha na Freddy Maro
Ongera watanzania kwa kuwekeza nchini kwani tunaweza lakini Mbona vifaa vya kijikinga hamjampa mh Rais naomba tuwe makini Rais Wetu tunampenda na tunamuhitaji
ReplyDeleteHongereni sanaMh Raisi,Hongera wawekezaji.Waziri wa Nishati yupo atwambie kama hiyo ni juisi?
ReplyDeleteHii safi sana,nimefurahi sana leo kwa kusoma habari hii. Watanzania tunatakiwa kifanya hivi kwasababu tunaweza kila kitu kufanya.Hata kodi wakisamehewa kwa muda ni sawa kabisa hawa wawekezaji wa ndani
ReplyDelete