Mmoja wa Mabalozi wa OXFAM, Shamim Mwasha akifafanua kwa undani namna ya ushiriki wa shindano hilo dogo litakavyofanyika hasa kwa kupitia Magazeti Tando (Blogs),Shamim alieleza kuwa shindano hilo litawahusisha wanataaluma wanaotumia mitandano,kupendekeza mwanamke ambaye amewahi kumsaidia kwenye kilimo kwa namna moja ama nyingine,kwa kujaza fomu zitakazokuwa zikipatikana kwenye Blogs mbalimbali ikiwemo Michuzi Media Group (issamichuzi.blogspot.com,michuzijr.blogspot.com na Mtaa kwa Mtaa.blog),Bongo 5,Blogs za Mikoa,Millard Ayo.com.Missie popular blog,8020fashions Blog.Shamim aliongeza kuwa shindano hilo limezindulia ili kuwasaidia wanawake katika kilimo na kuwaondoa katika lindi la umaskini.
 Pichani kulia ni Meneja wa ushawishi na utetezi  wa haki za kiuchumi wa Grow Tanzania,Bi.Mwanahamis Salim akifafanua zaidi kuhusiana na shindano hilo mbele ya Wanahabari kwenye mkutano wao uliofanyika mapema leo makao makuu ya OXFARM  jijini Dar,Mwanamisi alisema kuwa lengo kuu ni kuweka daraja kati ya wakulima walioko mashambani na Wanaoishi mijini na pia kutambua mchango wa mwanamke mkulima huyo,shoto ni Balozi wa shindano hilo,Shamim Mwasha.


Mwanahamisi alisema kuwa baada ya mchakato wa wiki mbili wa watu kupendekeza majina ya watu na kutuma habari zao, tarehe 17 mwezi huu zoezi litafungwa na kulipisha jopo la majaji ambalo litachagua tano bora na kuzionyesha habari zao kwenye mitandao ili zisomwe na zichaguliwe. December 5 jopo litakaa tena na kumwangalia mshindi. Tarehe 6 December ndipo mshindi atatangazwa na mashindano yatafungwa
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi ndani ya Ofisi za OXFAM,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kina dada hawa nimewakubali kwani hawana makuu na sisi wakulima tunawaona kama wenzetu (related to rural community).

    Mdau
    Mkulima Mdogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...