Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya Ufungaji wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza iliyotolewa na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile( hayupo pichani) kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini.
Afisa Mkuu wa Mipango wa Jeshi la Magereza, Bw. Boniface Mkumbo( wa tatu kushoto) akiteta jambo na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufungwa rasmi Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza mara baada ya kufunga rasmi Kikao hicho leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro( wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Haji Janabi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine( wa kwanza kulia) ni Mchambuzi Kazi Mkuu toka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
We mdau funga kifungo siyo unaonyesha sharubu za kifua, to be fair kwenye picha ya pamoja ukakifunga kifungo safii kabisa.
ReplyDelete