Assalaam alaiykum Ankal na timu yako,

Kaka mimi ni mkazi wa Kigamboni, tunakuomba utufikishie kilio chetu kisikike angalau watusaidie namna ya kutuondolea adhabu tuipatayo ya usafiri wa mabasi aina ya Daladala yaliyokuwa yanakuja kivukoni.

Hali imebadirika sasa tangu kuanza kwa ujenzi wa barabara kutokea eneo la Kivukoni,Mabasi hayo sasa hivi hayafiki kabisa Kivukoni yanaishia Mnazi Mmoja na Stesheni, hebu fikiria mtu ashuke kutoka katika pantoni atembee mpaka Mnazi Mmoja ndio apande gari ya kwenda buguruni au sehemu nyingine.

Kwa kweli hii ni adhabu kubwa sana kwa sie wakazi wa Kigamboni,kwa muda wangeweza kuweka ulinzi zaidi mabasi yakawa yanageuzia nyuma ya Ikulu mpaka hapo zoezi litakapo kwisha au ndani ya kituo kipya cha Mabasi hapa feri mpaka hapo njia itakapokamilika.

Kituo kipo tayari na uwekwe ulinzi ili kusiwe na uharibifu,nini faida ya kituo?? au daladala hazifai kutumia hiki kituo kwa muda? Ankal kama huamini,Naomba uje eneo hili la Feri majira ya asubuhi,Mchana au Jioni uone dhiki tunayoipata kina sie.

Hivi ni kweli kwamba viongozi hawalioni tatizo hili? Sasa kwa wenye uwezo wanapanda bajaji mpaka Mnazi Mmoja kwa 1,500/ kwa kichwa na kurudi ni hivyohivyo. Halafu sio jambo la wiki au mwezi ni zoezi la zaidi ya miezi 3!! 

Tufikishie kilio chetu hiki ndugu Ankal na timu yako kwa wahusika.

Ahsante
Mdau Mohamed wa Magogoni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa kweli kama serikali ina msaada kwa wananchi hawa ijaribu kuwapatia, leo asubuhi nimeshuhudia watu wakitembea kutoka posta ya zamani kuna bajaji zinapeleka watu ferry kwa sh. 500/= lakini unaona kabisa mtu hawezi kumudu hiyo mia tano anabidi akaze buti; mbaya zaidi kwa macho tu unaona wananchi wengi ni wa hali ya chini wengine wanamizigo na watoto migongoni. TAFADHALI SERIKALI SIKIA KILIO HIKI.

    ReplyDelete
  2. Ankal Michuzi,

    Kiukweli watu wengi hasa watumiaji wa barabara hizi zinazotengenezwa na kampuni ya Strabag tunaungana na mdau juu ya usumbufu na mateso ya HALI YA JUU unaotokana na ujenzi huu wa barabara. Kila mtu anajua kuwa ujenzi wa barabara ni muhimu kwaajili ya kuinua uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla. Ila pia ujenzi huu ungeweza kufanyika kwa njia ambayo itapunguza usumbufu uliokidhiri kwa wananchi. Mfano kituo cha kivukoni, mataa ya ubungo na barabara ya kimara kiukweli ni usumbufu wa HALI YA JUU. Kuna haja ya kamati ya usalama barabarani ya mkoa kukaa pamoja na kampuni hii ya ujenzi ya Strabag kuangalia uwezekano wa kuruhusu magari kupita vizuri angalau mida ya asubuhi watu wanapowahi makazini na jioni watu wanapotoka makazini. Kiukweli bila kufanya hivi ni usumbufu ulizidi sana ukiachilia mbali ajali zisizohesabika kwa wakazi wa maeneo wanaotumia barabara hizi.

    Viongozi husika inabidi kufunguka.

    Naomba kuwakilisha,

    Mdau.

    ReplyDelete
  3. Mtoa Makala hii Mdau Mohamed wa Magogoni na wachangiaji wawili hapo juu:

    Msubiri kuanzia mwaka 2014 mtakuwa ndani ya Usafiri wa mabasi ya DART.

    Suala hili ni la muda tu Mradi ukikamilika na hali yenu ya usafiri itakuwa imeimarika kwa kuwa na usafiri wa Kiwango cha Kimataifa kwa Mabasi yaendayo kasi badala ya KUTU za viti za mabati ya Mabasi ya ma-Toyota DCM za sasa!

    Huo usumbufu wa sasa ndio gharama za maendeleo yenu wenyewe,,,!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...