Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga moja ya nyumba ya waalimu katika shule ya sekondari ya Ikuti iliopo katika kata ya Ikuti,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mapema leo,akiwa sambamba na Ujumbe wake hawapo pichan,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro.Kinana na Ujumbe wake wako ziarani Wilayani Rungwe Magharibi mkoani Mbeya,ambapo kesho watakuwa wilaya ya Ileje kutekeleza Ilani ya chama,kukagua miradi ya chama na wanachi sambamba na kujua na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.
Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM pichani kati,Ndugu Abdulrahman Kinana
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme
kilichopo kwenye zahati ya Ikuti,katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe
mkoani Mbeya,Zahanati hiyo hapo awali ilikuwa ikitumia umeme wa Solar.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha
Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo,Kinana alizungumza
mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua tatizo sugu la Maji na
Barabara katika kijiji hicho,alichozaliwa Mbunge wa jimbo la Rungwe
Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa.Aidha kinana aliitahadharisha Serikali
katika suala zima la kuitaka iache urasimu na umangimeza katika
mipango ya maendeleo kwa Wananchi,aliongeza kuwa Urasimu na umangimeza huo
huwanufaisha zaidi wanaoshikilia fedha za miradi hiyo wakati wananchi
Wanaumia na kuteseka kwa kukosa huduma muhimu mbalimbali.Kama vile haitoshi Kinana aliongeza kuwa kama chama wataanzisha kampeni kabambe ya kupambana na huo Urasimu na Umangimez.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Wilayani Rungwe.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Wilayani Rungwe.
Wakienda kukagua moja ya bweni la kulala wanafunzi wa shule hiyo ya Ikuti
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro wakielekea kuonana na balozi balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha Ikuti,Bwa.James Mbasi ,pichani nyuma anaefuatia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Pichani
shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa
na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro
walipokuwa wakielekea kukagua jengo la bweni la kulala wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Ikuti,Wiayani Rungwe mkoani mbeya leo.
Anakal naomba niende nje ya mada ingawa sio sana.Wakati tunakua miaka ile ya 70,80 kulikuwa na gwaride linaitwa "CHIPUKIZI".Bado lipo hili?Tulikuwa tunagombania kweli kweli na lilikuwa burudani.Kama lilishapotea ufanyike utaratibu wa kulifufua kulingana na mazingira ya sasa tuliyomo.Na huko ndiko tulifundishwa UZALENDO tukiwa bado wadogo sana.Sasa hivi tuko 'BIZE' sana kupeleka watoto wetu kila aina ya so-called International schools(Angalizo:Sipingi hizi shule na Elimu kwa ujumla,ila elimu iendane na Uzalendo.Rais wetu ameongelea hili juzi Poland nadhani,watu kuitetea Tanzania)
ReplyDeleteDavid V
kuna mtu ameshauri kata zitafute jinsi ya kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi shule za kata hasa kwa wasichana kwa kujenga mabweni ya kuta za miti, zipigwe lipu ya kawaida tu na ziwekwe bati kama kata hazina uwezo kujenga nyumba za matofali. inasemekana kuna shule umasaini zimejenga mabweni ya 'manyata" na wanafunzi wanakaa shule na wanasoma vizuri tu. nimependa hili wazo na namuuliza mama rose migiro kama ataweza kupeleka hili jambo mbele zaidi kama agenda kwenye chama tawala na serikali za mitaa... lengo ni kuwa na majengo ya bei nafuu iwezekanavyo.
ReplyDelete