Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela mkoani Mbeya, ambako ataanza ziara rasmi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzipatia ufumbuzi.Pichani, Kinana na wajumbe wake wa sekretarieti ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea, kuanza safari ya kwenda Kyela. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ernest Kahindi
Kwaherini wakazi wa wilaya ya Nyasa,sasa tunaelekea wilaya ya kyela mkoani Mbeya.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wakiwa na shamra shamra wakati wakiusindiza ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana walipokuwa wakielekea Kyela mkoani Mbeya mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ina maana CCM waliingia Malawi ziwani bila visa wala nini DUH! aaaah natania kidogo wanandugu, pia nakumbushia iel issue yetu naona kama vile tunajisahaulisha vile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...