Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni  mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazia pia kuwa chama cha CCM ni chama imara,hivyo ni lazimaa lazima kiihoji serikali juu ya  pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za Wanachi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mtindo wa Kinana unatukumbusha enzi za msaragambo, hazikuwa mbaya.

    sesophy

    ReplyDelete
  2. Duuh.....hizo "gea" za Mzee Kinana hizo.....akiendelea hivi mpaka 2015....aah Ikulu ya magogoni itakuwa ya "sisiemu" bila shaka....katibu mkuu kubeba mtofali kama huo...tena anaupandisha "m-block" mpaka juu ....nadhani hii siyo tu kwaajili ya picha....hapo hiyo inaonekana kuwa Muheshimiwa anapiga kazi!

    Sijui kama CDM wanatafakari nini wakiona "speed za kinana" kama hizi....au sijui ndo bado wanatafakari huo "waraka wa siri"

    ReplyDelete
  3. wakati mwingine (japo si mara zote) siasa nayo inakuwa ni kama mchezo wa makosa vilevile sawa na "football" - yaani makosa ya mpinzani wako yanakuwa ni "opportunity" kwako kujipatia goli...hata kama si lazima sana ushinde mchezo wenyewe....lakini kadiri makosa ya mpinzani wako yanavyoongezeka na wewe kutumia udhaifu huo kupata magoli zaidi ndivyo inavyokupa uhakika wa ushindi....CDM wanahitaji kujipanga sana vinginevyo kwa kasi hii ya mchezo wa CCM ...huko 2015, kazi ipo!

    ReplyDelete
  4. Miji mingi naona mabati yana kutu inabidi wenyeji wajue yameexpire yanatakiwa mapya. Watafute kureplace na mabati yenye rangi.

    ReplyDelete
  5. "...yameexpire yanatakiwa mapya..

    Si rahisi...michakato ya kupata mabati mapys sio event, kama kunyesha mvua; ni process inayoptakiwa kupangwa kwanza. Kupanga ni kuchagua. Kula nyma au samaki siku hiyo au kununua mabati mapya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...