Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kushoto) akiongozwa na viongozi wa Kata ya Manzese kuelekea kwenye ukaguzi wa maendeleo ya Mradi wa Maji Safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Mivuleni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wakichota maji ya mradi wa maji safi na salama ya kisima wa Manispaa hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda (mbele kulia) akikagua kivuko kinachounganisha Kata ya Sinza na Kijitonyama, Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Mendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E mwishoni mwa wiki.
Mkandarasi wa Kampuni ya Drilling and Dam Construction Agency, Elzei Makaso (kulia) akimelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Magomeni Dosi, Dar es Salaam wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akizindua Mradi wa Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E, Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo (CHADEMA), Renatus Pamba.
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Kinondoni, Gonzalves Rutakyamirwa (kushoto) akimwelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (mwenye shati ya drafti) maendeleo ya mradi wa Maji safi na salama ya kisima unaotekelezwa kwenye Mtaa wa Mivuleni, Manzese, Dar es Salaam juzi wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwenye Kata tisa za Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Diwani wa Kata hiyo, Eliam Manumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. SIASA ZA KIWANGO CHA CHINI, INAMAANA WAKAZI WOTE WA KINONDONI WATACHOTA MAJI KUTOKA KISIMA HIKI! HAPANA NA HAIWEZEKANI.MAJI YOTE YA VISIMA DAR ES SALAAM SI SALAMA KWANI NI MKUSANYIKO WA MAJI TOKA JUU YA ARDHI AMBAYO TAYARI YANA KEMIKALI NA UCHAFU WA KILA AINA, CHA KUJIULIZA TANGU ONGEZEKO LA VISIMA DAR ES SALAAM UNYONYAJI WA MAJI TAKA KWENYE MAKAZI UMEPUNGUA KWA KIASI KIKUBWA, KWANINI?

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli ninyi viongozi wa Manispaa ya Kinondoni acheni kufanya kazi kwa kuzima moto. Mlikuja na kampeni ya usafi tena bw. Mwenda ulionekana kushiriki kisha ilipoishia haielewiki. Kazi ya kutoa takataka kwenye mitaro ni ya nani? Utakuta watu wa wilaya yako wanasafisha mitaro kwa kuweka juu ya barabara halafu, hakuna magari ya kubeba, mvua ikinyesha zinarudi tena kwenye mitaro. Ndug zangu acheni kuuza sura na kubembea kwenye viti, Wilaya yenu ni chafu, barabara zenyewe havijulikani kama ni lami au za vumbi mfano mzuri ni hizi mlizolamisha daladala/magari kuingia Makumbusho, Kijitonyama hata kuziwekea lami kama ile mliyodanyishia Akachube road ambayo sasa inamaandaki kibao, haileweki mmeshindwa kazi!!! Hamuoni wilaya .... barabara zinafagiliwa!!! Mh, unaongoza wilaya ya wasomi sasa msifanye viini macho mkidhani watu hawaoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...