MARY JOHN MWINGIRA
5.5.1946-21.11.2010
Leo ni Miaka 3 tangu ulipotuacha hapa Duniani kwa simanzi kubwa tarehe 21.11.2010. Ni kama juzi kwetu mama, kidonda hakijapona kabisa, uchungu mkubwa ndani ya  nyoyo zetu zimetawala kila saa mama. Ulijua kifo chako na ulikuwa unatuonea huruma sana ukijua tutakavyoumia.
”Samahani na poleni wanangu” yalikuwa ndio  maneno yako kila mara na hatukuwa tunaelewa kwa nini ulikuwa unasema vile.
Ulitufundisha kusali sala nyingi tukiwa wadogo na tunaamini  usemi wa Mapenzi ya Mungu yametimizwa mama.
Tutaonana siku ya Mwisho Paradiso!!!
 Tunaaminini upo karibu na MUNGU  kama ulivyokuwa hapa duniani .Ujumbe  wako mkuu uliotuachia tunajitahidi kuuteleleza  na kuishi katika  hilo “Upendo usio na masharti kati yetu wanao na wanaotuzunguka”.
Tunasema asante sana kwa malezi na maelekezo kuhusu maisha ambayo ulikuwa unatupa kila siku ukishirikiana na baba na ndugu na jamaa. Tunashukuru kwa Baraka za  MUNGU na  tunaamini kwa maombezi yako na baba tunamudu Maisha ya kila siku yaliyojaa Baraka tele.
Sisi wanao, wajukuu,mama yako, wakwe, Wadogo zako, shemeji zako , ndugu na Jamaa wote tuakumbuka na Kuusifu wema wako usio na kipimo. Tunakuadhidi kuundeleza kwa nguvu zetu zote na daima hatutakusahau Mama yetu na Rafiki yetu Mary John Mwingira


Ustarehe kwa Amani mama yetu Mpendwa!
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mama mwingira rest in peace

    ReplyDelete
  2. Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo, Mama ametuonesha njia ya kuishi duniani, tunaifuata. Upendo wa MUNGU uwafunike familia ya Mwingira

    ReplyDelete
  3. RIP MAMA MWINGIRA,Wote tu wasafiri, umetutangulia lakini wote tu njia moja. USTAREHE KWA Amani mama
    Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...