Maandalizi ya miaka 50 ya chuo cha uhifadhi na usimamizi wa wanyapori Mweka yakiwa yamekamilika tayari kungojea wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho.
 Wanafunzi wa chuo hicho wakichukua taswira katika banda la maonesho chuoni hapo.
 Maandalizi ya miaka 50 ya chuo cha uhifadhi na usimamizi wa wanyapori Mweka yakiwa yamekamilika tayari kungojea wageni mablimbali walioalikwa katika hafla ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho.
======  =======  ======
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

MWANASIASA nguli ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye anatajwa kuwania urais mwaka 2015, Waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu,Edward  Lowasa na Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk.Regnald Mengi ni  miongoni mwa watu mashuhuri walioalikwa jioni hii katika hafla ya  uchangiaji wa maendeleo ya Chuo cha Uhifadhi na Usimamizi wa  Wanyamapori,Mweka.

Zaidi  ya dola za kimarekani 3.6 bilioni sawa na sh. bilioni sita za
Tanzania,zinahitajika kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho,
kilichojengwa miaka 50 iliyopita.Katika harambee hiyo pia serikali
imewaita wabunge wote wa majimbo ya mikoa ya
Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga kushiriki uchangiaji huo.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,Dk.Freddy Manonge, ameiambia globu ya jamii
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye anayetarajiwa kushuhudia uchangiaji wa
chuo hicho ambacho kimepanga kupanua miundo mbinu yake kwa ajili ya
kuanza kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ujangili katika
hifadhi za taifa na maeneo tengefu yanayotishiwa na vita ya ujangili
wa tembo na faru.

Juzi,wataalamu wa usimamizi na uhifadhi wa wanyamapori kutoka nchi za
Scandinavia,Bara la Ulaya,Amerika na Afrika, walikutana mkoani
Kilimanjaro kujadili matumizi ya teknolojia mpya, iitwayo Forensic
Science Laboratory ambayo itatumiwa kuondoa utata wa kuwabaini
majangili wanaoendesha vitendo vya uharamia vya kuteketeza tembo na
faru kupitia taarifa za vinasaba.

Amesema kuwa chuo hicho kipo kwenye mkakati wa kupanua huduma zake
katika ukanda wa Afrika ili kuweza kuchukua wanafunzi kati ya 800 hadi
1000 kwa mwaka wa masomo ikiwa ni pamoja na kukiwezesha kumudu gharama  za manunuzi ya magari na vifaa vya kisasa vitakavyowawezesha wataalamu  na wanafunzi wanaohitimu mafunzo hayo kukabiliana na mbinu chafu za  watu wanaoendesha matukio ya ujangili.

Mbali ya ujenzi wa madarasa,miundo mbinu na ununuzi wa magari maalumu ya chuo hicho kikonge barani Afrika,serikali inatarajia kugharamia uingizwaji wa teknolojia hiyo ya Forensic Science Laboratory katika mitaala ya vyuo vyake vya uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori na utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...