Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa kadi ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account katika benki hiyo, Elianasa Marco Njiu,mkazi wa jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Nov 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa kwanza kupata mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...