Na Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye miji ya Shinyanga na Moshi watapambana vikali na kuburudika katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Shycom mjini Shinyanga na uwanja wa CCM Mkoa mjini Moshi siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza litakalofanyika Moshi zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya Malindi Band pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Kilimanjaro.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...