Mashabiki wa Simba wameendelea kutangaza ubabe kwa mashabiki wa Yanga baada ya kuwashinda kwenye mechi za mashabiki hao zilizochezwa jana kwenye miji ya Shinyanga na Moshi kupitia bonanza la Nani Mtani Jembe, lililoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambapo pote Simba walishinda. Hata hivyo Yanga waliweza kujipoza huko Moshi kwa kupata ushindi mnono kwenye michezo ya kufukuza kuku, kupiga penati kwenye goli dogo na kupiga danadana.
Shinyanga bonanza lilianza mwendo wa saa 9 alasiri ukitangulia mchezo wa kufukuza kuku ulitangulia ambapo mashabiki wa Simba waliibuka washindi dhidi ya Yanga. Baada ya hapo ulifuata mchezo wa kukimbia ukiwa umevaa gunia ambapo Charles Shija wa Simba aliibuka kinara kwa mikimbio 2 dhidi ya 1 wa Yanga. Ulifuata mchezo wa kuvuta kamba wanaume ambapo pia Simba walishinda yanga 2-1.
Baada ya mchezo huo kulifuata mechi kali sana kati ya mashabiki wa Simba wa soka wa mkoa wa Shinyanga na mashabiki wa soka wa Yanga, ambapo katika mechi hiyo simba walipata penati kipindi cha kwanza na mchezaji Iddi Mobi hakufanya ajizi na kukwamisha mpira wavuni.
Mpaka mapumziko Simba 1 Yanga 0, kipindi cha pili Yanga walikuja juu ili wasawazishe lakini bahati haikuwa kwao na kujikuta wanapachikwa bao la pili lililofungwa na Kulwa Mobi. Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na dakika 8 kabla ya kipenga cha mwisho walipata penati iliyotiwa nyavuni na Amani Rashid. hivyo mpaka filimbi ya mwisho Simba 2, Yanga 1.
Huko Moshi mashabiki wa Yanga walishinda mchezo wa kupiga dana dana na kupiga penati kwenye goli dogo, kufukuza kuku. Kwenye mchezo wa soka, mashabiki wa Simba walishinda kwa goli 2 – 1 na pia walishinda kuvuta kamba. Bonanza hilo lilipambwa na Malindi Band, Msanii maarufu wa bongo flava wa Moshi ajulikanae kama Majirani pamoja na wasanii wa kundi la Black Warriors.
Kupitia kampeni ya Nani Mtani Jembe, bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Timu za mashabiki wa Yanga na Simba zikimenyana uwanjani
ambapo Simba waliibuka washindi kwa bao 2-1. Ni ktk bonanza
la kampeni ya NANI MTANI JEMBE lililofanyika ktk viwanja vya
Shycom Manispaa ya Shinyanga jana.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Nanyie kama mna nia njema na soka la tanzania tunaomba muamke kidogo maana hamna hata haya,ni bora MJENGE VITUO VYA KUKUZIA VIPAJI VYA WATOTO WETU,,muone haya jamani toka lini mpira ukachezwa kwenye uwanja wa vumbi? Hiyo ni sawa na kuendesha gali lisilo na usukani,,nakama mnawapenda kweli hao simba na yanga muwejengee viwanja vya kisasa,ni aibu kubwa kwa timu za simba na yanga kutokua na viwanja vya kisasa,,hata RAIS WETU AMEWAAMBIA ni aibu kwa timu kama simba na yanga kutokua na viwanja vyao,,
ReplyDelete