Al-khayr Madrasa ilipokuwa mwanzo kabla ya kuuzwa
Al-khayr Madrasa ilipo sasa panapotakiwa kuendelezwa
Al-khayr Madrasa, iliyoanzishwa mwaka 1980, Buguruni Kisiwani jijini Dar es salaam, Tanzania, imelazimika kuhamishwa sehemu iliyokuwepo kwenda sehemu nyingine kutokana na uboreshaji wa miundombinu ya eneo hilo, mnunuzi wa Madrasa hiyo alinunua kwa Tsh. 30,000,000/= (Milioni thelathini) kutokana na udogo wa eneo.
Na nyumba ambayo imepatikana ni yenye namba ILALA/BUG/KISW/655. Ina thamani ya Shilingi 50,000,000/= (Milioni hamsini) na tayari zimeshalipwa zile Milioni Thelathini kwa makubaliano ya kumalizia deni la Milioni ishirini ifikapo Tar: 30/02/2014. Mkataba ambao umefanyika Tar:04/04 2013 . Shauri hilo limefanyika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Ilala.
MALENGO
Uongozi wa Al-khayr Madrasa unakusudia kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima, chekechea pamoja na muendelezo wa Madrasa. Hivyo basi ndugu zetu waislamu na wasiokuwa waislamu tunaomba kwa kila atakae guswa na jambo hili atusaidie kwa kadri ya uwezo wake ipatikane hiyo shilingi Milioni 20 tunayodaiwa na mwenye nyumba/eneo, kama inavyoonekana pichani: kwa mawasiliano zaidi wasiliana na uongozi wa madrasa:
O713-898686-Mussa Hamadi Ally
0713-574043-Uwessu Hamidu Belege
0716-178823-Lule Ally Ibrahim





kwa mtazamo wangu madrasa nyingi zimekuwa zinafunguliwa sehemu zisizofaa ukiangalia hata hilo jengo linalotaka kuendelezwa jinsi lilivyo haliwezi shawishi kuwa patakuja endelezwa kituo cha kulelea watoto yatima na chekechekea nadhani muwe na mtazamo endelevu eneo lenyewe kichochoroni hapo kweli patafaa matumizi hayo husika? kwa nini pasingekuwa eneo kubwa lenye nafasi hata eneo la kucheza watoto wakipumzika kudurus hata kama ingekuwa ni msingi umeanzishwa watu wangevutiwa kuchangia na hayo malengo yake yakatimia lakini hivyo palivyo panatisha ukipata wachangiaji labda pesa zao hawana pa kupeleka watu wanapenda kuchangia vitu vya maendeleo lakini kwa hapo sijui.tubadilike waislam tunapotaka kufanya kitu kiwe kweli kinadhihirisha hata kwa mtazamo sio ubabaishaji mwingi.
ReplyDeleteMCHANGIAJI HAPO JUU wewe ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kubadilika, na usiwatupie lawama w2 ambao upeo wao umefikia hapo,kama unadhani unayo mawazo mazuri kwa jamii hiyo yapeleke ili kuboresha zaidi,otherwise hawa watu wamejitahidi kiasi chao na wanahitaji surppot kutokea hapo walipo wamejitahidi kiasi chao...
ReplyDeletekatafuteni sehemu inayolingana na fedha ulizonazo
ReplyDelete