Shabiki maarufu wa Yanga Steven amejitosa katika fani ya filamu ambapo ataanza kuonekana karibuni akiwa katika muvi inayoandaliwa na Dr Cheni itayokwenda kwa jina la 'Nimekubali Kuolewa'. Steven alijipatia umaarufu ghafla baada ya mitandao kurusha video inayomwonesha analia baada ya timu ya Yanga anayoishabikia kufungwa. Kwa upande wa Dr Cheni ambaye ni msanii aliyeanza fani hii takriban miaka 15 iliyopita, anakuja kivingine baada ya kukaa kando kwa mwaka mmoja. Katika filamu hii pia kuna nyota kutoka China ambaye anakuwa Mchina wa kwanza kuigiza kwenye Bongo Movie. Angalia trela chini hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wewe ile tu Yanga imefungwa na Simba 5-0 kilio!

    Je, Steven mwanawane kucheza Sinema kwataka ujasiri pana matukio magumu ndani yake hivi utaweza?

    ReplyDelete
  2. Wachina!! mmmhhhhh

    ReplyDelete
  3. kazi nzuri.

    ReplyDelete
  4. Ukiwa na nia njia itapatikana.....unaweza bwanaaaa. Keep it up brother. Unaweza fanya mengi zaidi. Huu ni mwanzo.

    ReplyDelete
  5. Hahahaha!

    Mdau wa kwanza, Steven Mliaji atakuwa ni 'Komandoo wa Picha za Kihindi' ni vile Makomandoo wengine hadi wale wetu waliopo kwenye Kikosi cha Kulinda Amani Congo-DRC huwezi kupata anayelia kirahisi hata awe wa Kike.

    Lakini wale Makomandoo wa Sinema za Kihindi hulia kirahisi kama Steven wa Yanga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...