Mmiliki wa kampuni ya 2 Eyez Production na aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha television cha channel ten Bw. Frank Mtao (pichani), Jumamosi iliyopita ya tarehe 23/11/13 alifanikiwa kunyakua kiti cha uenyekiti wa chama cha jumuiya ya watanzania waishio New South Wales nchini Australia.

Katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Lethington uliopo kitongoji cha Summer Hill, mjini Sydney, Frank alifanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye ni mkazi wa muda mrefu katika jiji la Sydney Bw Christopher Banda kwa kura 55 dhidi ya 6 alizozipata Chriss.

Baada ya ushindi huo mzito, Frank aliwashukuru wanachama wote kwa kujitokeza kwa wingi na kufanikisha sherehe hizo za kufunga mwaka na uchaguzi na pia aliwapongeza wengine waliochagulia katika bodi yake ya chama hicho na kuhaidi watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwahaidi kuongeza jitihada za kuwakutanisha Watanzania hao na kusaidiana kwa kila hali!

Kwa upande wa msaidizi wa Frank yaani nafasi ya ukatibu ilikwenda kwa Louis ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa Tanzania Bw. S.H Amoni.

Kwa habari zaidi zinapatikana kupitia Facebook ya jumuiya hiyo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...