Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja
anayedaiwa kuwa ni mkazi wa KCMC amefariki dunia papo hapo jioni ya
jana baada kugongwa na gari aina ya Fuso na kuacha njia na kisha kumgonga
na kujeruhi wengine wawili.
Tukio hilo limetokea jana majira saa 12:30 jioni katika mtaa wa Posta jirani
kabisa na mgahawa wa Fresh Coach huku mwili wa marehemu huyo ukishuhudiwa ukiwa chini ya gari hilo kwa takribani saa 1 kutokana na
kukosekana kwa Winchi la kuinua fuso hiyo iliuweze kutolewa.
Mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio hilo wamesema mwanamke huyo alikuwa
ametoka katika shughuli za kibiashara katika soko lililopo mjini hapo.
Ripota wa Globu y jamii aliyokuwa maeneo ya jirani lilipotokea tukio hilo na alishuhudia gari
aina ya Fuso lililosajiliwa kwa namba T 209 AHA likiendeshwa na dereva
ambaye jina lake halijafahamika mara moja,likisababisha ajali hiyo iliyopelekea kifo cha Mwanamama huyo.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliosababishwa
na dereva wa Fuso hilo anayeonekana kabisa kuwa kalewa.
Watu wawili waliojeruhiwa kufuatia tukio hilo, ambao ni
dereva wa bodaboda na rafiki yake waliokuwa wamepaki pembezoni mwa
mtaa huo wakisubiri wateja.
Dereva wa Fuso hilo lililokuwa na maandishi yanayosomeka "AINULIWE
BWANA" anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC na taarifa
zaidi kuhusiana na tukio hilo zitatolewa mpaka pale upelelezi
utakapokamilika.
Mmoja wa Majeruhi katika ajali hiyo ambaye ni Dereva wa Bodaboda (kulia) akisaidiwa baada ya kutokea kwa ajali hiyo,huku pikipiki yake ikiwa haitamaniki.
Pikipiki nyingine nayo ni kama inavyoonekana.
Hili ndio lori lenyewe lililosababisha ajali hiyo.
Dereja wa Lori hilo (mwenye fulana nyeupe) akiwa ndani ya Gari la Polisi huku akijificha uso wake.
Mashuhuda eneo la tukio.
Namba za Usajili za Lori hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...