Na Mohamded Mhina wa
Jeshi la Polisi, Zanzibar
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 55, mkazi wa Kijiji cha Kidutani Gando mkoa wa Kaskazini Pemba ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 na baadaye kujitosa bahari kukwepa mkono wa dola.
Mzee huyo Muslih Mserembe, alikamatwa na wananchi waliokuwa wamekizingira kibanda chake kilichojengwa kwa miti, kuezekwa kwa makuti na kukandikwa kwa udongo wakati akimbaka binti huyo bila ya huruma. (Jina la binti huyo linahifadhiwa kwa usalama).
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12.00 alfajiri wakati binti huyo akiwafuatilia wenzake kwenda shambani kuokota maembe na ndipo mzee huyo alipomuona na kumuita.
Amesema baada ya binti huyo kumsogelea mzee huyo, alimwambia waingie ndani ya nyumba yake akidai kuwa angempatia maembe badala ya kuwafuata wenzake na ndipo alipombaka na binti kupiga kelele za kuomba msaada.
Kamishna Mussa alisema baada ya kelel hizo wananchi walikwenda nyumbani kwa mzee huyo na wakati wakiizingira nyumba yake, mzee huyo alitoka na kutimua mbio na kwenda kujitosa baharini lakini wananchi nao walijitosa humo na kumvua kama samaki.
Amesema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, wananchi hao walimpeleka katika kambi moja ya KMKM na ndipo Polisi walipofika na kumchukua kwa hatua zaidi.
Kamishna huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa binti aliyebakwa alikimbizwa katika Hospitali ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuendelea vizuri.
Kamishna Mussa ambaye amelaani vikali kitendo hicho, lakini amepongeza hatua za wananchi za kumkamata mtuhumiwa bila ya kumzuru na kumfikisha kwenye vyombo vya dola akiwa salama.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.
Hiki ni kitendo cha kulaaniwa kabisa. Hivi wazee wengine wakoje?
ReplyDeleteVitendo vya ubakaji wa watoto kila kukicha vinaripotiwa ni wakati sasa wa kutoa adhabu kali kwa wabakaji ama wote wafungwe maisha. Inasikitisha wengine wamefungwa maisha wakati wengine wako huru mtaani na hawafanyiwi lolote na wanarudia Kina Mama Nkya mko wapi? Wizara ya Mama na Mtoto inafanya nini tunawapoteza watoto wetu
ReplyDeleteWe Mserembe, ukitoka jela nakunyima pia na uraia wa Pemba.
ReplyDeleteKama unaweza kuishi baharini tutakuona.
HUO MTINDO WA KUBAKA WATOTO WADOGO UKO TOKEA ZAMANI ZA KALE,, NA HAKUNA HUKUMU YA MAANA, WATOTO WA KIKE NA WA KIUME WAMEKUA WAKIBAKWA NA KUCHANWA SEHEMU ZA SIRI, MIMI NAKUMBUKA NIKO MDOGO MIAKA HIYO NISHAWAONA WATOTO WENZANGU WALIOCHANWA,,, YAANI SIJUI WANAUME WAKOJE NI WATU WABAYA SANA. SIJUI WANA ROHO ZA VIPI. HUKO VISIWANI NDIO USISEME NA NDIO MAANA KUNA WASENGE WENGI. SEMA CHA KUSIKITISHA HAO WASENGE WAKISHAKUA WANAPATA WAKATI MGUMU KUTOKA KWA WANANCHI KWA KUONEKANA KWA NINI WANAFANYA VILE, NA KUNYANYASWA, KUCHUKIWA NA WANANCHI NK, BILA KUJUA NI NINI KILIWAPATA MPAKA WAKAAMUA KUWA VILE,,,,MBONA MAJANGA,,, KAMA HAIJAWEKWA HUKUMU YA MAANA HIKI KITENDO CHA UBAKAJI KITAENDELEA MILELE....
ReplyDelete