Marehemu Vicent Limoy wakati wa uhai wake ,akizungumza katika kika cha
kwa cha baraza la kwanza toka halmashauri hiyo kuongozwa na upinzani
muda mchache baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu meya wa halmashauri ya
manispaa ya Moshi.

======== ======== ==========
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.
CHADEMA manispaa ya Moshi kimepata pigo baada ya na naibu meya wa
manispaa hiyo na Diwani wa kata ya Kiboriloni(Chadema) Vicent Limoy
kufariki dunia ghafla leo mchana wakati akipatiwa matibabu katika
zahanati ya Jafary .
Meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael(Chadema) alithibitisha
kutokea kwa kifo hichona kwamba marehemu alifariki ghafla muda mfupi
baada ya kufika hosptalini hapo kwa ajili ya kutizama afya yake baada
kujisikia vibaya wakati akiwa shambani kwake.
“Mimi nimepokea taarifa hiyo dakika 30 zilizopita na kwa mujibu wa
taarifa za awali nilizopatiwa ni kwamba alienda kutizama afya yake
hapo zahanati baada ya kuhisi kifua kuwa kizito wakati akiwa shambani
kwake Msalanga.”alisema Michael.
Alisema mara ya mwisho kuzungumza naye kuhusu ugonjwa ilikuwa ni
wakati wamesafiri kwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya mazungumzo na
serikali ya nchi hiyo ambapo alimwambia kuwa amekuwa akisumbuliwa na
ugongwa wa miguu(Gauti).
Michael ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema manispaa ya Moshi alisema
chama kimepokea kifo hicho kwa mshutuko mkubwa kutokana na ukweli
kwamba marehemu ndiye alikuwa muasisi wa chama katika manispaa ya
Moshi.
“Chadema manispaa tumepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha huyu
mzee,mbali ya kuwa muasisi wa chama pia alikuwa kiungo muhimu kama mtu mzima kwa wanasiasa ambao ni vijana bila ya kujali itikadi za
kisiasa.”alisema Michael.
Alisema marehemu aliwahi kushika nafasi mbalimba za uongozi ndani ya
chama hicho ikiwemo nafasi ya uenyekiti wa Chadema manispaa ya Moshi
kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kuiacha nafasi hiyo kwa ridhaa yake na
kumpendekeza yeye(Michael) kushika nafasi hiyo.
Alisema pia marehemu alikuwa diwani wa kata ya Kiboriloni kwa vipindi
vitatu mfululiozo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005,2005 hadi 2010 na 2010
kuelekea 2015 huku akiwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho
katika manispaa ya Moshi.
“Naweza sema alikuwa ni kiongozi mwandamizi ndani ya Chadema na pia
ameshikilia nafasi ya naibu meya kwa vipindi vyote vitatu na mara ya
mwisho alichaguliwa kwa kura zote ambazo zilipigwa na madiwani wa
Chadema na CCM”alisema Michael.
Alisema siku chache zilizopita Meya Michael alikuwa amemuagiza
marehemu Limoy jijini Dara es Salaam kumwakilisha katika mazungumzo na Ujerumani juu ya kukabiliana na uzalishaji wa taka ambapo pia
alitiliana saini ya makubaliano hayo.
“Ni majuzi tu alienda kusaini hayo makubaliano ,nab ado alikuwa
hajanipa feedback(mrejesho) ya kile kulichoendelea kule katika
makubaliano na nilikuwa nimepanga kukutana nae siku mbili hizi
“alisema Micahel.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosptali ya rufaa ya
KCMC na kwamba hadi sasa chanzo cha kifo chake hakijafahamika .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...