Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliofika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho leo,ambapo Kamati ya Chama hicho imeamua imeamua kuwavua nyadhifa mbali mbali baadhi ya viongozi wa Juu wa Chama hicho akiwepo Mh. Zitto Kabwe. Wengine pichani toka kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Udhamini wa Chama hicho, Sylvester Kanyansi Masinde, Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lisu na viongozi wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Na Chadema Blog
KAMATI kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande.
Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu kilichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejulikana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema. Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2.
Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.
CCM oyeee chadema mmeula wa chuya,mm ni chadema damu lakini kwakitendo mlichokifanya hakiyamungu ZITTO na wezake hao watachukua uuumaaati wa wana chadema wooooteee mtabaki nyie tu viongozi wa juu tu,,nawaomba CCM iwachukue kwa mikono miwili hawa watu coz ni watu muhimu sn kwenye taifa letu na ccm mkifanikiwa kuwapata hawa watu basi mkaee mkijua hamtohitaji KUPIGA KAMPENI maana ushindi nnje nnje,, the mdudu Kaka K,
ReplyDeleteMh! This is the real meaning of Movement for Change?
ReplyDeleteIt looks like a childish propaganda.
Udini gani huo baina ya Dk. Mkumbo na Zitto, mbona hawa dini tofauti?
Yaani hawa wamechanganyikiwa kweli. Zitto Kabwe na Kitilla Mkumbo wamefanya kazi kubwa sana kuhamasisha vijana. Hata mie ambaye si mwanachadema hao watu wawili ndio walikuwa wananipa imani cha chadema, kuwa ni chama kinachhongozwa kimipango na kitaalamu. Hata sisi ambao si wanachadema,tunataka Chadema yenye nguvu kwa manufaa ya nchi yetu.
ReplyDeleteMhe.Zitto Kabwe vua pajama la Chadema vaa nguo za rangi ya kupendeza karibu sana kwetu sisi M,
ReplyDeletemlango uko wazi
NAMI NANG'ATUKA.CHADEMA WAS TO BE TUMAINI LA WATANZANIA ILA MAAMUZI YA KUFINYANGA DEMOKRASIA KWA KUMTETEA KAMANDA MBOWE NA DKT SLAA SI SAWA.NIMESOMA WARAKA WALA SI HATARI KIASI HICHO.UDINI NA UKABILA UKO WAPI?
ReplyDeletenimeijua chadema na kuanza kuifatilia baada ya kumfuatilia kwa makini zito ,kwa hili lilotokea nimeishiwa nguvu si jui tumuamini nani, KWELI CHADEMA KUNA UNAFIKI, ZITO TUPO PAMOJA NITAKUFATA UENDAKO KWASABABU BADO NAKUAMIN UNAPENDA UKWELI NDO MANA WAMEKUFANYIA HIVYO ILI WAONEKANE WAZURI,jana bbc tar 22, wamesema wameanza kukuandama ulipo onyesha nia ya kugombea uwenye kiti, wanachuki hao na ni wanafki mwngapi wao wanakosea, chama kinamwenyewe, watu mbaka wana kadi mbili lakin hatukusikia,ni mwana nusu chadema kuanzia jana sina imani na uongoz ngoja tuwaachie chama sasa
ReplyDeleteNini Kumfuta nyadhifa bwana! Bado ni Mwenyekiti wa kamati Muhimu bungeni inayo mpa jina na heshima.
ReplyDeleteWachaga Oyeeeeeee!
ReplyDeleteChadema Oyeeeeree!
Arusha Oyeeeeeeeee!
Moshi Oyeeeeeeeeee!