Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo..
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
“Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini,” amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali na kuongeza:
“Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013),” ameongeza.
Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
Your Legacy will always be remembered. R.I.P Dk Mvungi.
ReplyDeleteTaifa limepoteza mtu wa muhimu sana na mwanazuoni mahiri kweli katika nyanja ya sheria na siasa za Tanzania hasa wakati huu kuelekea Uundwaji wa Katiba mpya.....RIP Sengondo....Poleni sana wanafamilia, M/Kiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Hon. Jaji Warioba & wajumbe wa Tume
ReplyDeleteMay his soul rest in aternal peace Dr Mvungi..ni ngumu kuamini lkn ndio njia yetu sote. Haki na sheria vichukue mkondo tumechoshwa na mauaji ya namna hii. Mdau.
ReplyDeleteTanzania sio salama kuishi.
ReplyDeleteTukaishi wapi?
DeleteDr Mvungi,kuondoka kwako ni pengo lisilozibika kwa familia yako. Nawaombea Mungu awape faraja familia. Kuondoka kwako pia ni pigo kubwa kwa Taifa la Tanzania na hasa wapenda maendeleo na demokrasia.Tutakukumbuka,na historia ya Tanzania haitaacha kuandika mchango wako mkubwa wa kazi uliyokuwa ukiifanya pamoja na wajumbe wengine wa tume ya Katiba kabla ya kifo chako.Upumzike kwa amani.
ReplyDeleteYaani hawa wauwaji! Mungu wangu! ipokee roho ya huyu baba na uwape ujasiri ndugu na familiya! Sasa kweli! tanzania tunaenda wapi kama ni kukatana mapanga tu! Kisa siasa na umasikini wa akili na mwili!
ReplyDeleteThis is so sad!
tumempoteza mwanasheria mzuri tanzania.bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.R.l.P Dr.Mvungi
ReplyDeletePoleni sn wanafamilia na kwa taifa letu,na hao waliohusika wafungwe MAISHA ili iwe fundisho kwa wakatisha maisha ya watu wengine,,RIP Dr Mvungi,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA,,ijapokua kuna baadhi ya wadau wanakeleka na mm kusema nipo huku uingereza,mm sitoacha kusema nilipo coz situsi kwangu,,nawapendeni wote huko nyumbani na mkaee kwa amani na upendo,
ReplyDeleteMay God rest him in evelasting peace! Acha ushamba na ulimbukeni kuwa Uingereza ni utumwa tu wabongo na Afrika kwa ujumla washayajua maisha ya UK.au Ulaya au US watu mnapigika tu na kazi za kijinga hamna la maana lolote mnalofanya siyo huko Ulaya au US wala nyumbani bongo.TZ au Afrika kuna maisha ya heshima ukisoma unapata kazi ya staha ya taaluma yako siyo huko hata waliosoma hakuna kazi wanaishia kufanya kazi za kijinga.TZ au Afrika hata wafanyabiashara wa kati wana maisha ya mazuri kuliko watu wa ughaibuni!Tumeshawajua huko ughaibuni mnateseka tu na mengi kazi za kijinga hali ya hewa mbaya baridi tu mtindo mmoja stress life na wengi na akili zimewaluka!
ReplyDeleteRest in peace DK.Mvungi
ReplyDeleteMungu akulaze mahala Pema peponi. Nakumbuka Ulikuwa head prefect wetu Mzumbe sekondari baada ya Hamisi Kibola na kurithiwa na Nyamajeje Wegoro.
ReplyDeleteR.I.P Dr. Mvungi.
ReplyDeleteJamani jeshi la polisi liangalie haya mambo ya hualifu yamezidi sana.
Tumepoteza International figure, natamani wauaji wawe chini ya himaya yangu nipewe panga, sime, rungu kubwa, bisibisi then niwafanye mishikaki wanajiona!
ReplyDeleteRIP Dr. Mvungi tutakukumbuka sana daima.
Poleni familia na nccr kwa msiba huu mzito
ReplyDeleteDr Mvungi Mungu kakupenda zaidi kiukweli ulipokuwa mgeni rasmi pale graduation ya Canossa uliwapa watoto mie naita wosia mzuri siamini ulikuwa unawaaga hivi kweli uliweza hata kumwish mwanao Adrian? Mungu aipe familia yako faraja itoshayo maana ni Mungu tuu aweza kuwafariji.
ReplyDeleteKWANI KUWA KWAKO UINGEREZA INAUHUSIANO GANI NA MADA ILIYOPO HEWANI? WACHA MAKIDAI!!!!!!!!!! WENGI TUPO UGHAIBUNI NA HATUSEMEI HAPA.
ReplyDeleteMUNGU AILAZE ROHO YA DR MVUNGI MAHALA PEMA PEPONI-AMINA.
Mheshimiwa Rais, hali nadhani, hivi sasa ni tete. Urais wa mwaka 2015 ni majanga. Tafadhali, hebu angalia, cheki na Usalama wa Taifa, what is going on? . Urais hautafutwi kwa hivyo.
ReplyDeletePole sana wanapenda amani, poleni sana wanafamilia...hii kali..TZ hakutamaniki tena. Watu wanaohitajika ndio wanaondoka hivyo... Tz tutabaki na akina wachumia tumbo. Maendeleo hakuna tena ... Loooooooo! TZ yetu unatuacha hivi hivi.. Mwalimu alikulea vema, ukakua vema ..vipi sasa umetugeuka?
ReplyDeleteMmm ni Uchungu MKUBWA haswa ukilichukulia ndio lako...Uchungu mkubwa ni kwa Mke pia,si rahisi kwa hali ya kawaida.Pole Rais wetu mpendwa Tunakuombea na Taifa letu pia..Mungu awape ujasiri kwa Watoto na Mama pia. MUNGU MBARIKI RAIS WETU,IBARIKI TANZANIA YETU,WABARIKI NA VIONGUZI WOTE NA WATANZANIA WOTE..
ReplyDeletewe dogo wauingereza hapo juu hujakua bado ukikua utaacha
ReplyDeletePoleni wafiwa kwa kupoteza mpendwa wenu..
ReplyDeleteTukio hili lisaidie kuimarisha usalama wa makazi tunayoishi kwa ulinzi shirikishi na kusogeza ofisi za polisi karibu na makazi yetu.
TUJIFUNZE KUVUMILIANA, KUNA WATU AU FAMILIA IMEPOTEZA BABA YAO,BABU YAO,KAKA YAO,MWANA FAMILIA WAO,KIUNGO CHAO NA YOTE ZAIDI MAMA MVUNGI KAFIWA NA MUME HAPA. SASA NI VEMA KUWAPA POLE WAFIWA HAWA KWA MOYO MMOJA NA KUEPUKA KUWEKA MALUMBANO YASIO NA TIJA. MTU KUTOA RAMBIRAMBI ZAKE NA KUSEMA ANAPOISHI SIONI KAMA KUNATATIZO HAPO. HAJATUKANA BALI ANAONYESHA/KUFAHAMISHA WAFIWA NA WENGINEO WOTE WAMEOGUSWA NA MSIBA HUU KUWA RAMBIRAMBI HIZI ZINATOKA SEHEMU FULANI ,ON OTHER HAND NI KUWA MSIBA HUU UMEGUSA WOTE HATA WALIO MBALI KIHIVYO. KILA MTU ANAHIYARI YA KUSEMA SALAM ZAKE ZINAKO TOKEA. .WHETHER ZINATOKA MWANZA, KIGOMA. ,KARATU, USA,UAE, RUSSIA. .NK. PIA TUSISAHAU NI HIYARI YA MTU KUCHAGUA ANAPOISHI WETHER UTUMWANI AU LAA NI MAAMUZI TUU ALMRADI HAYAKUTURUBU WEWE. NA WALA SI UTOTO AU USHAMBA.
ReplyDeleteRIP DR. MVUNGI. .Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yako mahali pema na akupe pumziko la milele. Amen
Mdau USA.