Dkt. Sengondo Mvungi, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi ambaye pia ni Mjumbe wa tume ya Katiba (pichani), amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake jijini Dar es salaam na amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiofahamika ambao habari za awali zinadai kuwa ni majambazi.
Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi Taifa, Mhe Moses Machali, ameiambia Globu ya Jamii muda mfupi uliopita kwamba Dkt Mvungi alijeruhiwa vibaya sana usiku (wa kuamkia leo) saa 6.Mhe Machali amesema taarifa zilizopatikana ni kwamba walimkata mapanga hasa kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu, na kwa sasa yupo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
"Wana NCCR-Mageuzi na Watanzania wote tupeane pole kwa uvamizi wa Dkt Mvungi. Tumwombee na kumtakia apate kupona haraka", alisema Mhe. Machali, ambaye pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini, akiongezea kuwa hali yake ni mbaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Uwii Mungu wangu mbona majanga. Jamani inasikitisha sana, Polisi tafadhali lisimamieni hili wahalifu hao wakamatwe na ku adhibishwa.

    Majambazi hao waliiba kitu gani nyumbani na Dr. Mvungi? au walienda tu kwa nia la kumjeruhi? kama walienda kwa nia tu ya kumjeruhi basi hao sio majambazi wa kawaida. Tunategemea polisi watupe majibu.

    Pole sana Dr, Mvungi, tunakuombea upone haraka. Poleni wana familia kwa kuuguza.

    ReplyDelete
  2. Many questions an ansewred, Get well soon ma dady

    ReplyDelete
  3. Dr wa watu amewakosea nini? Jeshi la polisi naamini litatoa taarifa kamili.

    ReplyDelete
  4. Pole Dr wetu mungu akujalie upone haraka. Kwa nini haya yanajirudia? Inanikumbusha mwalimu wangu Dr Khidu Makubuya aliyetwambia anakaa cumpus makerere for security reasons though ana bungalow Muyenga. Watu wetu muhimu please serikali hakikisha wanakaa maeneo salama japo mmejiuzia tengeneza mengine kila mtu ajue hapa kuna serikli hata kama ni Mapinga etc. Natumaini mungu atakuponya

    ReplyDelete
  5. Pole sana rafiki yetu kipenzi chetu,mtetezi wetu.Mungu akupe nguvu dr.Mvungi.Wana familia pia poleni sana.amaungu atamsaidia atapona tu.Sisi rafiki zake ,tumeandaa dua ya pamoja na watoto yatima Alhamisi jioni,Ilala DSM.Mungu atamnusuru kama alivyomnusuru nabii Yunus katika tumbo la samaki, kama alivyomponyesha nabii ayub baada ya kuumwa miaka tele,na akarudi kuwa mwenye kuvutia ,INSHAA ALLAH.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...