Msanii wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila akisherehekea mwaka mmoja toka aache kutumia mihadarati katika hafla maalumu iliyoandaliwa kwa wanaopata matibabu ya kutumia madawa ya kulevya katiuka hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam wikiendi ilopita. Ujumbe hapo ukiwa "Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana".
Ray C akiwa na wagonjwa wengine katika hafla hiyo
Ni furaha tupu kwa Ray C kuweza kutimiza mwaka bila kutumia mihadarati





Ray C ni mzuri sn? Naomba tuwasiliane kama hutojali kupitia hapa hapa kwa mjomba Michuzi,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA,
ReplyDeleteRay C bibie jitahidi zaidi!
ReplyDeleteAma kweli 'Maisha bila unga inawezekana' !!!
Isipukuwa ukumbuke ya kuwa ''Unga Kinyama cha hamu'' ! ikiwezekana jitahidi kukaa mbali sana na hao jamaa ambao hawaja pona kabisa kama wewe kwa kuwa unaweza ukapata maambukizi mapya na ukazama tena kirahisi!
Maana msisikie 'mzigo' una kishawishi sana!
mbeba box maarufu kakakuona...hehe watu bwana washamba kweli kwani lazima useme upo uingereza.
ReplyDeleteMdau wa 3 juu,
ReplyDeleteSound ni muhumi ktk haya mambo ya mawindo!
Ray C hayupo pabaya bado ni Staa hivyo ana fit kwa watu kama kakakuona aliyepo mbele huko.
mimi namtetea kakakuona, nikuwa kutaja alipo Uingereza ndio ktk kutafuta point sasa wewe unataka aseme yupo Gairo ama Ludewa kweli azma yake atafanikisha?
Mdau kakakuona,
ReplyDeleteRay C kitu mwanawane lakini Unga mbona majanga!,,,Alisha anza kuwa kama Bibi Kizee.
Ray C kwa utumiaji unga alipondeka vibaya sana!
ReplyDeleteUnga msala wamaisha,
Unga albadiri ya Kihindi,
Unga bunduki ya maangamizi tuuepuke.
Unga ulimharibia Whitney Houston na uimbaji wake. Ray C kaa safi ni bahati iliyoje kupatiwa nafasi ya kuishi bila kufungwa na madawa ya kulevya.Usichezee hiyo fursa.
ReplyDeleteWeye mdau unaemtetea Mdudu KAKAKUONA nakushukulu sn,nimefurahi na kuguswa na maneno ya busara uliosema,kwanza umepatia kitukimoja ambacho sikutalajia hiyo GAIRO iko ndani ya mkoa wangu wa MOROGORO,so thanks verymuch for that,,na bila kujali kama ww ni M au Mwanaume naomba upokee ushauri wangu na ufanyie kazi,1 kama unasoma soma kwa bidii zaidi faida utaziona baada ya masomo,kama unafanya kazi jitume pasipo na mfano na uwe mwaminifu,,ipo siku bosi wako atakuita ofisini kwake,mshahara juu na cheo juu,hiyo ndio siri ya mfanyakazi bora na umwamini mungu kuliko uchawi,kama umeowa au umeolewa mpende sn mkeo au mmewako,na kama ni kiongozi wa serikali au wa siasa achana na mambo ya ruchwa,ulevi,ngono chafu,,kisha jiulize why nchi yangu haipigi hatua kubwa za kimaendeleo wakati mali tunazo na kwanini watanzania wenzangu hasa wa vijijini hawapati huduma muhimu kama nnazopata mimi,basi utajikuta unatafuta vituo vya TV na RADIO na kuanza kupiga kampeni za haki kwa wote inawezekana pasipo kupigana wala kuchukiana,,asante sn Mdau ulie nitetea,INSHAALLAH mungu akipenda 1day tutatafutana,siku njema kwako na kwa wadau wote wa Mjomba Michuzi blog,mm naipenda sn Tanzania yangu,vipi wenzangu tupo pamoja au?
ReplyDeleteHongera sana Ray C, sikujui lakini nilibahatika kusoma habari zako humu na kuona picha zako ni kweli ulikuwa umechakaa.
ReplyDeleteHii ni changamoto kubwa kwa vijana woote watumiaji na wasiotumia.. kwani wewe ni kioo cha jamii, basi kama umeweza kustay clean kwa mwaka mmoja ni vizuri kuwa unaende hizo sehemu ambazo kuna waathirika na kuwashuhudia kuwa unaweza ukapiga U TURN...na kwa wale walio clean wasijeshawishika kutumia ili kuonekana COOL au kupunguza ukali wa maisha.... BIG WELL DONE AND KEEP IT UP MAMAA!!!
watu wanaingia kwenye mtandao bila kujua kuwa dunia ni kama kijiji......najua siyo vibaya sana kusema uko wapi wakati unatumia "plat form" hii ya Ankal kuwasiliana au kutoa comments.....However, ni ushamba sana kurudiarudia kusema niko Uingereza, Japan etc...kwakuwa dunia ni kama kijiji so it makes no difference kama uko Kanyigo, Nyarugusu, mbamba bay au hata kama uko Denver Co(USA)....Ni vizuri tuelimishane pia humo humo - Nadhani hapo Ankal sija chafua hali ya hewa, au?
ReplyDeleteEnyi waazimia kutotumia madawa ya kulevya, jihadharini na "triggers" zinazowasukuma nyuma kurudia hiyo tabia mbaya, chafu na mauti!
ReplyDelete