Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Mkurugenzi wa utafiti Dkt. Ladislaus
Chang’a walishiriki katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo kati ya
Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Serikali ya Norway yaliyofanyika mjini
Warsaw Nyumbani kwa Balozi wa Norway nchini Poland tarehe 21 Novemba,2013.
Kutoka kushoto ni Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO) Bw.Michel Jarraud, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe; Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, Msaidizi wa Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa
Duniani (WMO) Bi. Elena Manaenkova na kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi katika mkutano wa COP 19 huko Warsaw Poland.
Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani alipomtembelea
Mheshimiwa Rais katika hoteli ya Bristol tarehe 20 Novemba 2013, alimjulisha
kuhusu msaada huo na kwamba Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya awali katika
kutekeleza mpango huo kwa imani kwamba TMA itasimamia vyema utekelezaji wake na
kupata matokeo mazuri yatakayosaidia kupanuliwa kwa mpango huo katika nchi
zingine za Afrika. Kwa upande wake Mheshimiwa Rais alimshukuru Bw. Jarraud kwa
misaada ambayo WMO inaisaidia Tanzania na aliahidi kwamba serikali itaendelea
kuisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa ili iweze kutekeleza majukumu yake na
kushiriki vyema katika program za WMO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...