WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anatamani kuona Serikali za Mitaa hapa nchini zinasimamia maendeleo kuanzia ngazi ya chini kwa kushirikiana na sekta binafsi ikiwa ni njia ya kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Ametoa kauli hiyo huo leo mchana (Jumatatu, Novemba 25, 2013) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa ushirikiano baina ya Mamlaka za Serikali za Mitaa za China na Tanzania ulioanza leo jijini Dar es Salaam.
“Ni muhimu tukaanzisha ushirikiano huu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa kwa sababu usimamizi wake unakuwa karibu zaidi na wananchi kuliko ilivyo hivi sasa”, alisema.
Kuhusu ujio wa magavana, mameya na wafanyabiashara wapatao 71 kutoka majimbo manne ya Shandong, Liaoning, Shaanxi na Jilin, Waziri Mkuu alisema ujio wao umekuja wakati muafaka kwani unasaidia kujenga mahusiano ya karibu zaidi na wananchi kwenye ngazi ya chini kuliko inavyokuwa kuna mahusiano kwenye ngazi ya Kitaifa peke yake.
Ngugu zangu watanzania tusiichee hii nafasi ya kua KARIBU na TAIFA KUBWA KAMA HILI LA CHINA HII ni bahati ilioje ndugu zangu,,na sisi kama watanzania twende na kasi yao coz hawa watu hawana mchezo wanapokua kazini so tuwape ushilikiano wa hali ya juu sn ili wawe na imani zaidi na sisi,,na pia sivibaya tukiingiza lugha yao ya KICHINA kwenye mashule yetu yote hapa Tanzania nzima,,hawa watu wanatutakia mema sisi watanzania huwezi kufananisha na WAZUNGU,,wazungu ni kama mdudu kupe anavyo mnyonya mbuzi au kondoo damu,,tuamkeni watanzania wakati ndio huu wa kuchapa kazi kisawawasa ili tuijenge nchi yetu iwe imara zaidi jivunie utanzania wako popote ulipo,,asanteni sn wadau kama mmeipenda changieni zaidi mawazo yenu,kwa wasio nielewa, sorry to them,,,naitwa MDUDU KAKA KUONA or mbeba box
ReplyDeleteWell said "Mdudu K".....
ReplyDelete