Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Yussuf Khamis (Mwenye shati la drafti katikati) katika picha ya pamoja na Wafanyakazi Wastaafu wa ZBC walio mstari wa mbele, katika Hafla maalum ya kuwaanga iliyofanyika Bungi Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Wastaafu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC wametakiwa kutoa ushirikiano wao pale unapohitajika ili kulifanya Shirika hilo kuzidi kusonga mbele.

Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Yussuf Khamis katika Hafla maalum ya kuwaanga Wafanyakazi Wastaafu wa Shirika hilo iliyofanyika Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema licha ya Wastaafu hao kuwa nje ya kazi ushauri wao utazingatiwa ili kuliimarisha zaidi Shirika hilo. “Nakuombeni musijitenge moja kwa moja na Shirika kama mna ushauri wowote basi karibuni Ofisini ili kuliendeleza Shirika letu ” Aidha Yussuf amewataka Wafanyakazi wa ZBC kuzidisha mashirikiano miongoni mwao ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.

Kwa upande wao Wastaafu hao waliushukuru uongozi wa Shirika kwa kuweza kuwaandalia Hafla maalum ya kuwaaga jambo ambalo walidai baadhi ya taasisi hawafanyi hivyo.

Aidha waliiomba Serikali kuzidi kuyaboresha maslahi ya Wafanyakazi ili Wanapomaliza muda wao wa kulitumikia taifa waweze kumudu maisha yao vyema. Katika Hafla hiyo Jumla ya Wafanyakazi Wanne waliagwa na kukabidhiwa zawadi baada ya muda wao wa Utumishi kumalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...