Uwezo ni neno la Kiswahili lenye maana ya ‘kipawa au umahiri’. Uwezo ni mradi wa miaka minne wenye lengo la kuboresha ujuzi katika kusoma na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 6-16 nchini Kenya, Tanzania na Uganda, kwa kutumia njia bunifu kwenye kuleta mabadiliko ya kijamii ambayo yanatokana na raia wenyewe na kuwajibika kwa umma. Kwa mwaka huu zoezi la upimaji limeanza tangu tarehe 30 Oktoba 2013. Hapa kuna baadhi ya picha za matukio ya zoezi la upimaji manispaa ya Singida.
Mratibu wa Uwezo, Mkoa wa Singida, Bw. Amos Nkuwi (Kulia), akitoa maelezo juu ya zoezila upimaji KKK, kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kindai, Bw. Athman Masudi Maganga (kushoto) huku akiangaliwa na Mratibu wa Uwezo Wilaya ya Singida Manispaa, Bibi Zuhura Karya (kati-nyuma) na Bi. Shamim Hatibu, mkusanya taarifa wa Uwezo, Mtaa wa Kindai, Singida Manispaa.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kindai, Bw. Athman Masudi Maganga (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya matumizi ya dodoso la upimaji wa stadi za KKK, kutoka kwa Mratibu wa Uwezo Wilaya (Manispaa ya Singida), Bibi Zuhura Kayra (kati). Aliye upande kulia ni Bi. Shamim Hatibu, mkusanya taarifa wa Uwezo, Mtaa wa Kindai, Singida Manispaa.
Mwandishi wa makala za elimu (gazeti la the Guardian), Bw. Masozi Nyirenda, akikagua daftari la mmoja wa wanafunzi wa Darasa la Pili wa Shule ya Msingi Manguanjuki, Manispaa ya Singida, ikiwa ni sehemu ya zoezi la upimaji wa stadi za KKK linaoendeshwa na shirika la Uwezo.


Hongereni sana, hii itawasaidia watoto wetu kujua kusoma, kuandika na kuhesabu na pengine ikawa chachu ya kuwafanya wapende shule na kuzingatia masomo
ReplyDeleteAngalao kuna sehemu wameanza kuchukua hatua kuliokoa taifa letu kwenye janga la elimu. Mungu awazidishie kwani mmeanzia kwenye ngazi nzuri.
ReplyDelete