MAREHEMU MRS MAUA
MPANKULI
Familia ya
marehemu Maua Mpankuli tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Ndugu, Jamaa,
Marafiki, Wafanyakazi, Majirani na watu wote kwa ujumla waliojitoa kwa hali na
mali katika msiba wa mpendwa wetu aliyeaga dunia tarehe 1 Novemba, 2013 huko
Uingereza na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
tarehe 9 Novemba, 2013.
Tunapenda
kutoa shukrani zetu za kipekee kwa wafuatao:
* Madaktari na wauguzi wote wa hospitali ya St James ya Leeds,
Uingereza kwa jitihada zao kubwa za kujaribu kuokoa maisha ya marehemu.
* Jumuiya ya Watanzania wote walioko Uingereza na sehemu zingine za
dunia waliojitolea kwa hali na mali hadi kuweza kuusafirisha mwili wa marehemu
kutoka Uingereza hadi Tanzania kwa
mazishi.
* Uongozi na waumini wa Kanisa la Christ Temple of Worship Leeds
Uingereza kwa maombezi na ushikiano wao.
* Uongozi na waumini wa Kanisa la RCCG la Leeds, Uingereza kwa ushirikiano wao.
* Uongozi na
waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Church, Dar es Salaam kwa huduma za
kiroho wakati wote wa msiba na katika mazishi ya marehemu.
* Kampuni ya Hugh Gooding Funeral Services ya Leeds, Uingereza
iliyoshughulikia kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Leeds hadi Dar es Salaam
kwa mazishi.
* Wafanyakazi wote waliowahi kufanya kazi na marehemu katika Hospitali
ya Muhimbili, Dar es Salaam.
*Jamii na
viongozi wa Issamichuzi blog. Asanteni kwa kuturuhusu Kutumia mtandao wenu.
Tungependa
sana kuwashukuru kila mmoja wenu kwa majina lakini kwa ajili ya wingi wenu tunaomba
mpokee shukrani zetu hizi za kipekee kwa ujumla wenu.
Mwenyezi
Mungu awazidishie baraka zake nyingi kwa Huduma zenu mlizotoa. Asanteni sana.
Waefeso 1: 15 – 16.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...