Kamishina wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Mama Aida TESHA, akitoa nasaha na kufungua rasmi maonyesho ya sanaa zilizotengenezwa na watumiaji walio kwenye matibabu ya dawa za kulevya kupitia “Sober House”.
Mkurungenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa, Alliance Française, Ndugu Sullivan BENETIER akitoa neno la ufunguzi na ukaribisho wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kazi za sanaa yaliyoandaliwa na watumiaji walio kwenye matibabu ya dawa za kulevya kupitia “Sober House”.
Mmoja wa watumiaji wa dawa za kulevya walio katika matibabu kupitia Sober House akitoa maelezo kuhusu kazi zake za sanaa kwa mgeni rasmi Mama Aida TESHA wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya sanaa yaliyofanyika katika ukumbi wa Alliance Française.
Kamishina wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Mama Aida TESHA akiwa katika picha ya pamoja na Kamishina wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya kwa upande wa Zanzibar, Bibi Kheriyangu KHAMIS (kulia) na Mkurungenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa, Alliance Française, Ndugu Sullivan BENETIER, wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya sanaa yaliyoandaliwa na watumiaji walio kwenye matibabu ya dawa za kulevya kupitia “Sober House”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Lingine la kuwachangia ndugu zetu waliopata madhara ya Matumizi haya ya ziada ni kuwa:

    1.Binaadamu hawezi kupata happiness ama furaha kwa umiliki wa vitu, ama matumizi ya kitu Fulani bali happiness ama furaha huja kwa kujitambua na kujielekeza binafsi yaani PSYCHOLOGICAL REDEMPTION and SELF DEVELOPMENT.

    Kamwe umiliki wa vitu ama matumizi ya vitu haviwezi kuleta faraja ama furaha kwa kuwa KAMA KUNA UMILIKI AMA KUPATA na pia KUNA KUKOSA, HIVYO UNAPOKOSA NDIO UNAKUWA HUJAJIKIMU.

    Tuangalie kitu kama Mali au Fedha, unaweza ukawa na lengo la kutafuta LAKI MOJA, ukiipata utakusa hutosheki utatafuta zaidi na zaidi na hakuna Tajiri anayetosheka kwa kipato.

    Hivyo zaidi ya umiliki wa mali ama vitu pia matumizi ya ziada kama Unga na ulevi wowote haviwezi kuleta faraja ya kweli ama furaha BALI HULETA HAYO KWA MUDA TU (tuangalie Mlevi baada ya kulewa siku inayofuata hupata 'hang over' ambayo inakuwa kitu kama 'karaha fulani' hivi, ni kuwa ile faraja ya muda imekwisha muda wake baada ya Ulevi kwisha) kwa kuwa faraja na furaha ya kweli huja kwa kujitambua na kujielekeza binafsi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...