Tangu kuanza kuchanganya kwa maendeleo ya Teknolojia Tanzania, tumeona makampuni mengi yakizaliwa siku hadi siku, kila moja likiwa na lundo la huduma wanazotoa kwa wateja wao. Iwe kwa yale ya simu, yale ya kibenki, yale ya kutengeneza programu na hata yale ya kuuza majina ya website (Domain names), wote hawa wamejikitia kuhakikisha mteja anapata anachokitaka.

Kitu ambacho mengi ya makampuni haya yemeshindwa kufahamu ni kuwa, je huyu mteja ANATAKA NINI? mteja hanunui huduma ama bidhaa kama bidhaa, bali ni faida/thamani (Value) inayokuja na ile huduma au bidhaa. Chukulia mfano, wewe ni Bank na unatoa huduma ya kibenki kwa mtandao (Online banking), mteja anayeamua kutumia huduma hii ya kibenki toka kwako, siyo kwa sababu anataka kuwa na akaunti ya bank au kutuma pesa tu, bali nini kinakuja na hii huduma.
 

Kwa mfano, binafsi ni mpenzi wa Bank X kwa sababu Bank hii ina huduma bora kwa mteja pindi ninapopata tatizo, endapo utapata tatizo kwenye matumizi ya Bank X, basi muda wowote ukipiga simu,kwanza hautakiwi kungoja kwa muda mrefu, pia tatizo lako litapatiwa ufumbuzi hapohapo bila kulipeleka kwa wa ngazi za juu (High first contact resolution rate). Na hivi ndivyo vitu ambavyo mteja anavihitaji.



Tukirudi kwenye ulimwengu wa Tehama, siku hizi kuna watoa huduma hii wengi mnomno, kila kona ya mtandao wamejaa, ila je wengi wa hawa wanafahamu nini mteja anahitaji? Kitu cha msingi kufahamu ni kuwa, ili kufanikiwa kwenye utoaji wa huduma yoyote, lazima muelekeo wa mawazo ya mtoa huduma yawe sambamba na mahitaji ya mteja, wakati wewe unafikiria HUDUMA mteja yeye anafikiria THAMANI ya huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...