![]() |
| Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Anne Makindaakihojiwa na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani |
Mkutano wa nane uliwaokutanisha maspika wanawake duniani umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York huku mjadala mkubwa ukiwa ni mkakati wa usawa wa kijinsia kuwa sehemu ya malengo endelevu ya milenia baada ya 2015.
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami amekutana na kufanya mahojiano na miongoni mwa waliotoa mada katika mkutano huo, spika wa kwanza mwanamke nchini Tanzania Anna Makinda ambaye pamoja na mambo mengine anasema anazungumzia suala la mabadiliko ya sheria ya ndoa nchini humo inayoruhusu msichana mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.Spika anasema mlolongo wa mabadiliko ni mrefu kulikoni? Kwanza Makinda anaanza kwa kueleza mjadala mkuu wa mkutano huo. Kusikiliza bonyeza hapa http://www.unmultimedia.org/ radio/kiswahili/2013/11/spika- makinda-asema-mabadiliko-ya- sheria-ya-ndoa-yana-mlolongo- mrefu/



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...