Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linasikitika kuwatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam, Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani kuwa, tangu Jumamosi ya Tarehe 23/11/2013 alfajiri Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu ulipata hitilafu baada auto-transfoma ya (high lift pump) moja kati ya tatu kuungua hali iliyosababishwa na hitilafu ya umeme.
Kutokana na hitilafu hiyo, uzalishaji Maji umepungua toka wastani wa lita 80,000,000 hadi lita 50,000,000 kwa siku. Hali hii itaathiri upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Wakati matengenezo yanaendelea maeneo yafuatayo yataathirika; MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, CHUOKIKUU, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.
transformer imepelekwa kwa wakandarasi kwa ajili ya kwenda kusukwa na Matengenezo yanategemea kuchukua wastani wa siku kumi (10)
Kwa wale watakao pata maji tunaomba mtumie kwa uangalifu na kuhifadhi kwa matumizi ya lazima.
KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022 5500 240-4
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...